Swali: Ikiwa nitampa mtoto wangu jina la baba yangu, je, hili ni katika kumfanyia wema?
Jibu: Huenda hili likawa katika kumfanyia wema, na huenda baadhi ya baba wasilipende hilo. Kwa hiyo kumpa jina kwa namna hii kunaweza kuwa katika kumfanyia wema na huenda lisiwe katika hayo. Kumfanyia maiti wema na ihsani ni kwa kumuombea du´aa, kutekeleza ahadi yake na kumheshimu rafiki yake. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa na muulizaji:
”Je, bado kuna jambo katika kuwafanyia wazazi wangu wema ambalo naweza kuwafanyia baada ya kufa kwao?” Akasema: ”Ndiyo; kuwaombea du´aa, kuwaombea msamaha, kutekeleza ahadi yao, kumuheshimu rafiki yao na kuunga udugu ambao hauungwi isipokuwa kupitia kwao.”
Hakutaja katika hayo kumpa mtoto jina la baba.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
- Imechapishwa: 10/10/2026
Swali: Ikiwa nitampa mtoto wangu jina la baba yangu, je, hili ni katika kumfanyia wema?
Jibu: Huenda hili likawa katika kumfanyia wema, na huenda baadhi ya baba wasilipende hilo. Kwa hiyo kumpa jina kwa namna hii kunaweza kuwa katika kumfanyia wema na huenda lisiwe katika hayo. Kumfanyia maiti wema na ihsani ni kwa kumuombea du´aa, kutekeleza ahadi yake na kumheshimu rafiki yake. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa na muulizaji:
”Je, bado kuna jambo katika kuwafanyia wazazi wangu wema ambalo naweza kuwafanyia baada ya kufa kwao?” Akasema: ”Ndiyo; kuwaombea du´aa, kuwaombea msamaha, kutekeleza ahadi yao, kumuheshimu rafiki yao na kuunga udugu ambao hauungwi isipokuwa kupitia kwao.”
Hakutaja katika hayo kumpa mtoto jina la baba.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
Imechapishwa: 10/10/2026
https://firqatunnajia.com/kumpa-mwanangu-jina-la-baba-yanu-ni-katika-kumtendea-wema/