Swali: Nina mtoto wa kiume nyumbani haswali. Nimezungumza naye na nimempiga lakini hakujirekebisha. Je, inajuzu kumfukuza nyumbani?
Jibu: Ni juu yako kujitahidi katika kumrekebisha. Ikiwa hatorejea, basi inajuzu kumfukuza na kumuweka mbali. Lakini kujitahidi kumrekebisha, hata kwa kumtia adabu na kumpiga, ni bora zaidi kuliko kumfukuza. Huenda Allaah akamuongoza kupitia sababu zako. Kwa sababu ukimfukuza huenda akapata mambo yaliyo mabaya zaidi. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:
“Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba, wapigeni kwa ajili yake wakiwa na miaka kumi na watenganisheni katika malazi.”
Hivyo ameamrisha kuwapiga na wala hakuamrisha kuwafukuza.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/188)
- Imechapishwa: 24/02/2026
Swali: Nina mtoto wa kiume nyumbani haswali. Nimezungumza naye na nimempiga lakini hakujirekebisha. Je, inajuzu kumfukuza nyumbani?
Jibu: Ni juu yako kujitahidi katika kumrekebisha. Ikiwa hatorejea, basi inajuzu kumfukuza na kumuweka mbali. Lakini kujitahidi kumrekebisha, hata kwa kumtia adabu na kumpiga, ni bora zaidi kuliko kumfukuza. Huenda Allaah akamuongoza kupitia sababu zako. Kwa sababu ukimfukuza huenda akapata mambo yaliyo mabaya zaidi. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:
“Waamrisheni watoto wenu kuswali wakiwa na miaka saba, wapigeni kwa ajili yake wakiwa na miaka kumi na watenganisheni katika malazi.”
Hivyo ameamrisha kuwapiga na wala hakuamrisha kuwafukuza.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/188)
Imechapishwa: 24/02/2026
https://firqatunnajia.com/kumfukuza-mtoto-asiyeswali-nyumbani/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket