Kuleta Takbiyr moja ili kuwahi Rak´ah nyuma ya imamu kwenye Rukuu´

Swali: Baadhi ya watu wakati imamu anapokuwa katika swalah hali ya kurukuu huja kwa haraka, kisha mmoja wao huleta Takbiyr mbili; Takbiyr ya kufungulia swalah na Takbiyr ya kwenda katika Rukuu´; na baadhi yao huleta Takbiyr moja tu. Ni ipi hukumu ya hilo?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah kwa maamuma anapokuja na imamu yuko katika Rukuu´ ni kutoharakisha. Bali atembee hali ya kuwa na utulivu na heshima, kisha aingie katika safu pamoja na imamu. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kufanya hivo. Alete Takbiyr ya kufungulia swalah akiwa amesimama, kisha alete Takbiyr ya kwenda katika Rukuu´ wakati anainama kwenda Rukuu´. Ikiwa atatosheka na Takbiyr ya kuingia katika swalah tu, inamtosheleza ili aweze kuwahi Rak´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/151)
  • Imechapishwa: 05/03/2026