Swali: Je, mjamzito anayefungua kwa kuchelea juu ya mtoto wake anaweza kulinganishwa na yule anayefungua kwa mfano ili kumuokoa mwingine? Kwa maana ya kwamba anapaswa kulipa tu siku hiyo au anapaswa pia kulisha chakula?

Jibu: Ndio, inajuzu kwa mtu kufungua ili kumuokoa mwingine kutokana na maangamizi ikiwa hali inalazimisha afungue na hawezi kumuokoa isipokuwa kwa kufungua. Basi anaruhusiwa kufungua na atalipa baadaye.

Swali: Je, analazimika kutoa kafara ya kulisha chakula sambamba na kulipa?

Jibu: Kuhusu kafara, sikati kauli kwa jambo hilo. Ama kulipa, anapaswa kulipa.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/409-410)
  • Imechapishwa: 18/02/2026