Swali: Mwenye kutaka kuupata ule muda wa saa ya mwisho ya siku ya ijumaa kwa ajili ya kuomba du´aa na kumuomba Allaah – je, inamlazimu awe katika sehemu aliyoswali ´Aswr, anaweza kuwa nyumbani au katika msikiti mwingine?

Jibu: Dhahiri ya Hadiyth ni ujumla na kwamba mwenye kuomba du´aa katika wakati wa kujibiwa, basi inatarajiwa ajibiwe katika saa ya mwisho ya siku ya ijumaa, inatarajiwa ajibiwe. Lakini ikiwa anangoja swalah katika msikiti anaotaka kuswali Maghrib, basi hilo ni lenye kustahiki zaidi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… ilihali yuko amesimama akiswali.”

Mwenye kungoja yuko katika hukumu ya mwenye kuswali, hivyo kuwa katika mahali pa swalah ni karibu zaidi na kujibiwa kwake. Basi anayengoja swalah yuko katika hukumu ya wanaoswali. Ikiwa ni mgonjwa akafanya hivyo nyumbani kwake basi hapana neno. Au mwanamke nyumbani kwake vivyo hivyo, hukaa akingoja swalah ya Maghrib katika mahali pake pa swalah. Au mgonjwa katika mahali pake pa swalah na aombe du´aa katika alasiri ya ijumaa, inatarajiwa kujibiwa. Hilo ndilo lililowekwa katika Shari´ah. Akitaka kuomba du´aa, basi aende mapema msikitini anaotaka kuswali Maghrib, aketi akingoja swalah na aombe du´aa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/270)
  • Imechapishwa: 21/02/2026