Kuanza mihadhara na sherehe mbalimbali za kidini kwa kusoma Qur-aan

Swali: Ni yepi maoni yako kufungua mihadhara kwa kusoma Qur-aan tukufu? Je, hii ilikuwa ni miongoni mwa desturi za Salaf?

Jibu: Sijui kitu cha wazi juu ya hili. Isipokuwa ni kwamba ilikuwa ni miongoni mwa ada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapokusanyika na Maswahabah zake basi anasoma Qur-aan au anasomewa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kitendo ulichouliza ni katika sampuli hii. Hatujui kizuizi juu ya hilo. Ndani yake ipo kheri nyingi. Ni uzinduzi juu ya yale yanayonufaisha kutoka katika Qur-aan. Kitu bora cha kuyafungulia maneno ni Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall).

Check Also

Kusoma Qur-aan au kuomba du´aa?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Du´aa hairudishwi nyuma kati ya adhaana na …