Kilichokatazwa ni mwanamke kuyatembelea makaburi sana tu?

Swali: Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah amewalaani wanawake wenye kuyatambelea makaburi sana.”

Hakusema:

“… wenye kuyatambelea makaburi.”

Matamshi ya kwanza yamekuja kwa njia ya wingi na hivyo inakuwa chenye kukatazwa ni wanawake kuyatembelea sana makaburi.

Jibu: Kumekuja upokezi wa pili unaosema:

“Allaah amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi.”

Upokezi huu unafasiri:

“… wenye kuyatambelea makaburi sana.”

Makusudio inakuwa wanawake kukatazwa kuyatembelea kabisa, sawa ikiwa atayatembelea sana au kidogo.

Huu ni utata umesemwa na wale wenye kujuzisha mwanamke kuyatembelea makaburi. Lakini hata hivyo ni lenye kurudishwa kutokana na dalili ya upokezi wa pili:

“Allaah amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi.”

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2106
  • Imechapishwa: 01/07/2020