Swali: Je, kuna dalili ya baadhi ya walinganizi kutofautisha kati ya ´Aqiydah na mfumo wa kulingania kwa Allaah kwa njia ya kwamba ´Aqiydah yao ikawa ya Salafiyyah na mfumo wao katika kulingania ima ikawa ni wa ki-Ikhwaaniy au ki-Tabliyghiy?

Jibu: Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ادْخُلُوا فِي السِّلْمِ كَافَّةً

“Enyi mlioamini! Jisalimisheni kikamilifu.”[1]

Ni lazima kuufanyia kazi kwa pande zake zote. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):

فَلَمَّا زَاغُوا أَزَاغَ اللَّـهُ قُلُوبَهُمْ

“Pindi walipopotoka, basi Allaah akazipotosha nyoyo zao.”[2]

Sisi si wenye kuleta vurugu katika dini hii. Ni lazima kuufanyia kazi Uislamu kwa pande zake zote bila kutenganisha kati ya misingi na matawi. Hiyo ni Bid´ah waliyozua, kama alivosema Haafidhw Ibn-ul-Qayyim katika kitabu chake “Swawaa´iq-ul-Mursalah”, yaliyozuliwa na al-Aswamm na Ibn ´Ulayyah; waliogawanya dini katika misingi na tanzu. Vinginevyo dini yetu yote ni misingi. ´Ibaadah zetu ni sehemu katika ´Aqiydah yetu na mambo yetu ya biashara ni sehemu katika ´Aqiydah yetu. Allaah hakuteremsha dalili yoyote juu ya mgawanyo huu. Baya zaidi kuliko haya ni kuigawanya dini katika maganda na nyama – mgawanyo huu ni Bid´ah ya kisasa.

Sisi tunamfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika ´Aqiydah na ulinganizi. Uongofu bora ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 2:208

[2] 61:5

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 392-393
  • Imechapishwa: 23/06/2025