Swali: Je, katika dini kuna Bid´ah inayoruhusiwa? Ni nini maana ya maneno ya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh):
“Bid´ah nzuri iliyoje hii!”?
Jibu: Hakuna katika dini Bid´ah inayoruhusiwa na wala Bid´ah inayochukiza. Bali zote ni upotofu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Bid´ah nzuri iliyoje hii!”
Haya ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo hakuna katika dini Bid´ah inayoruhusiwa wala inayopendekezwa. Bali Bid´ah zote ndani ya dini ni upotofu.
Ama yale ambayo baadhi ya watu huyaita Bid´ah, kama vile kujenga shule au minara ya misikiti, haya si Bid´ah. Bali ni mambo yaliyosababishwa na haja. Kwa hivyo ni katika mambo ya kheri na ya kujikurubisha. Minara ni kwa ajili ya kufikisha sauti ya adhaana isikike kwa watu, shule ni kwa ajili ya kufundisha Qur-aan na Sunnah na sehemu za kuwahifadhi masikini ni kwa ajili ya kuwasaidia watu, haya yote si Bid´ah. Bali ni katika mema na matendo ya kheri.
Ama kuhusu maneno ya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh):
“Bid´ah nzuri iliyoje hii!”
maana yake ni kwa upande wa lugha. Alipowakusanya watu waswali Tarawiyh nyuma ya imamu mmoja, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tayari alikuwa amefanya hivyo kwa masiku machache, kisha akaacha kwa kukhofia isije ikafaradhishwa juu yao. Baada ya kufariki Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na pia kufariki Abu Bakr (Radhiya Allaahu ´anh) ndipo ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) akaona ni vyema kuwakusanya watu waswali pamoja kwa imamu mmoja, kwa sababu walikuwa wakiswali kwa makundi tofauti msikitini. Akawakusanya nyuma ya imamu mmoja, jambo ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alishalifanya hapo kabla na sasa hakuna tena khofu ya kufaradhishwa kwa sababu wahy umekoma. Kwa hiyo akasema:
“Bid´ah nzuri iliyoje hii!”
kwa maana kwa maana ya lugha. Kwa sababu maana ya Bid´ah kwa mujibu wa lugha ni kitu kipya kisichokuwa na mfano wake hapo kabla. Kwa hiyo Tarawiyh hii ambayo aliwakusanya nyuma yake na wakaendelea juu yake ni Bid´ah kwa upande wa lugha, si kwa upande wa dini. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliifanya, kuihamasisha na akawaswalisha nyusiku kadhaa. Kwa msemo mwingine sio Bid´ah. Bali ni kujikurubisha na kumtii Allaah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3292/حكم-تربية-شعر-الراس
- Imechapishwa: 05/10/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3292/حكم-تربية-شعر-الراس
Imechapishwa: 05/10/2026
https://firqatunnajia.com/ipo-bidah-inayoruhusiwa/