Inafaa kumswalia na kumuobea msamaha mwenye kujiua?

Swali: Kuna mtu amejiua. Je, inajuzu kwa mtoto wake kumuombea msamaha kwa Allaah, kumuombea du´aa na kumtolea swadaqah?

Jibu: Ndio, kwa sababu ni muislamu. Amefanya dhambi kubwa. Ni muislamu. Hajatoka katika Uislamu. Anatakiwa kuombea du´aa, msamaha na kuswaliwa. Ataamiliwe kama waislamu wengine. Isipokuwa tu mtawala wa waislamu na watu wenye hadhi katika jamii ndio ambao hawatakiwi kumswalia. Lengo ni ili kuwashtua wengine. Si kwamba ni kafiri. Lengo ni ili kuwashtua wengine ili wasifanye kama alivyodanya huyu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (11) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/14466
  • Imechapishwa: 14/10/2017