Swali: Mke wangu amezaa watoto wanne na tangu miaka minne iliyopita hawezi tena kushika mimba. Madaktari wamekubaliana kumfanyia upandikizaji wa mbegu kwa njia ya kitabibu. Hali ni kwamba huduma hiyo haipo katika hospitali zetu za serikali isipokuwa Jeddah, naye amekataa kufanyiwa operesheni hiyo. Ni ipi hukumu?

Jibu: Upandikizaji wa mbegu kwa njia ya kitabibu umejuzishwa baadhi ya wanazuoni wa zama hizi kwa masharti muhimu na tahadhari kali ili yasitokee aliyoyaharamisha Allaah (´Azza wa Jall). Hata hivyo mimi ni miongoni mwa waliochukua msimamo wa kunyamazia jambo hilo na ninashauri kuacha kufanya hivyo, kwa sababu huenda ukafungua mlango wa shari usio na mwisho.

Ikiwa hawezi kuzaa tena, basi watoto wanne waliopatikana wanatosha na himdi zote njema anastahiki Allaah. Aidha anaweza kuoa mke wa pili, wa tatu au wa nne na Allaah atamruzuku watoto wengine kupitia mwanamke mwingine. Hivyo kuliacha jambo hilo ni bora zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/192)
  • Imechapishwa: 20/02/2026