Hukumu ya damu yenye kumtoka mwanamke baada ya kuoga

Swali: Ninaona kwamba ninapooga baada ya kumalizika kwa hedhi yangu na baada ya kukaa muda wake wa kawaida – nao ni siku tano – wakati mwingine hutoka kiasi kidogo sana cha uchafu mara tu baada ya kuoga, kisha baadaye hakutoki tena kitu chochote. Sijui, je, nichukue ada yangu ya siku tano tu na kilichozidi kisihesabiwe kisha niswali na kufunga bila tatizo au niihesabu siku hiyo kuwa ni katika siku za hedhi ambapo niswali wala nisifunge? Hali ya kuwa jambo hili halinitokei kila mara, bali baada ya takriban kila hedhi mbili au tatu. Naomba unifafanulie.

Jibu: Ikiwa kinachokutoka baada ya twahara ni majimaji ya njano au ya rangi ya udongo, basi hayo hayahesabiwi kuwa ni kitu. Bali hukumu yake ni kama mkojo. Ama ikiwa ni damu iliyo wazi, basi hiyo inahesabiwa kuwa ni katika hedhi na hivyo inakupasa kurudia kuoga. Kwa sababu imethibiti kutoka kwa Umm ´Atwiyyah (Radhiya Allaahu ´anhaa) – naye ni miongoni mwa Maswahabah wa kike wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – kwamba alisema:

”Tulikuwa hatuhesabu majimaji ya njano na ya rangi ya udongo baada ya twahara kuwa ni kitu.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/214)
  • Imechapishwa: 24/02/2026