Haikuthibiti “al-Qadiym” katika majina ya Allaah

Imaam at-Twahaawiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“[Allaah] ni wa kale bila ya kuwa na mwanzo.”

Neno wa kale (al-Qadiym) halikuthibiti kuwa ni katika majina ya Allaah. Limezushwa na wanafalsafa. Lililothibiti ni “wa mwanzo” (al-Awwal) na “wa mwisho” (al-Aakhir). Haya ni majina mawili ya milele na yenye kudumu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/50)
  • Imechapishwa: 07/06/2020