201 – ´Aliy bin Hujr ametukhabarisha: Ismaa´iyl ametukhabarisha, kutoka kwa Yuunus, kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakrah: Ashajj bin ´Asr amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alinambia: “Una tabia mbili anazozipenda Allaah.” Nikasema: “Ni zepi?” Aakasema: “Uvumilivu na haya.” Nikasema: “Je, ni ya tangu zamani au zimejitokeza?” Akasema: “Ni tangu zamani.” Ndipo akasema: “Himdi zote njema anastahiki Allaah ambaye ameniumba na tabia mbili anazozipenda .”[1]

[1] Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Adab al-Mufrad” (454).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 130
  • Imechapishwa: 29/09/2026