Eda ya mwanamke aliyeachwa talaka tatu

Swali: Ni ipi eda ya mwanamke mwenye kutalikiwa na mume wake talaka tatu?

Jibu:’

وَالْمُطَلَّقَاتُ يَتَرَبَّصْنَ بِأَنفُسِهِنَّ ثَلَاثَةَ قُرُوءٍ

“Wanawake waliotalakiwa wangojee kwa nafsi zao Quruu´ tatu.” (02:228)

Kwa maana ya hedhi tatu au twahara tatu kutokana na tofauti. Kwa hali yoyote ni lazima kupatikane mara tatu. Aayah hii imeenea, ni mamoja kwa mwanamke mwenye kutalikiwa mara tatu au talaka rejea. Ni yenye kuenea.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (65)
  • Imechapishwa: 16/11/2014