Swali: Je, ni sahihi ya kwamba imani haiwezi kukamilika ikiambatana na maasi? Je, imani inaweza kukamilika pamoja na mtu kuburuta mavazi [Isbaal] na kunyoa ndevu na kusikiliza muziki?

Jibu: Yaonekana kuwa hamfahamu kile mnachoambiwa. Maasi yanaipunguza imani. Kuburuta mavazi, kunyoa ndevu na madhambi mengine yote yanaipunguza imani. Upande mwingine mambo ya utiifu yanaizidisha imani. Imani inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi. Dhambi zote zinaipunguza imani.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_07.mp3
  • Imechapishwa: 01/06/2015