Swali: Mwanamke ana mimba ya mwezi wa sita. Daktari amemshauri kuwa huenda kipomoko kitakufa karibuni au kitazaliwa kikiwa na ulemavu. Pia daktari amemshauri atoe mimba na ameongeza kuwa kichwa cha kipomoko ni kikubwa. Nini maoni yenu?

Jibu: Wajibu ni kutokitoa kipomoko na awe na dhana njema kwa Allaah. Mwisho wake utakuwa mwema – Allaah akitaka.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/204)
  • Imechapishwa: 20/02/2026