Swali: Je, inaruhusiwa kuswali swalah ya kujitolea moja kwa moja baada ya swalah ya ijumaa?

Jibu: Sunnah baada ya ijumaa ni kuswali Rak´ah nne. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuwa ataswali baada ya ijumaa, basi na aswali nne baada yake.”

“Mnaposwali baada ya ijumaa basi swalini nne.”

Sunnah ni kuswali kwa Tasliym mbili baada ya ijumaa. Kufanya hivi ndio bora. Akiswali kwa Tasliym moja inatosha. Lakini lililo bora ni nne.

Vilevile imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikuwa akiswali nyumbani kwake baada ya ijumaa Rak´ah mbili. Lakini jambo lake ni yenye kusisitizwa zaidi, kwani aliamrisha nne. Kwa hiyo jambo ni lenye kusisitizwa zaidi. Hivyo Sunnah na lililo bora ni kuswali Rak´ah nne, ni mamoja iwe msikitini au nyumbani kwake, kwa Tasliym mbili baada ya ijumaa.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/269)
  • Imechapishwa: 21/02/2026