Anataka kufanya Tayammum ili awahi swalah ya mkusanyiko

Swali: Vipi ikiwa mtu atafika na wakati wa swalah umeshafika na si mwenye wudhuu´, je, inafaa kwake kufanya Tayammum ili aweze kuwahi kuswali kwa mkusanyiko?

Jibu: Haijuzu kwake kufanya Tayammum ili aiwahi swalah ya mkusanyiko. Bali ni lazima ajitwaharishe kwa twahara ya maji, hata kama swalah ya mkusanyiko itampita.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/340)
  • Imechapishwa: 21/11/2026