Anakhofia akirejesha haki kwa warithi basi kutatokea matatizo makubwa zaidi

Swali: Baba yangu aliapa na akakanusha haki za watu wengine katika mashamba ya mitende, ardhi na mengineyo. Sasa baadhi ya wenye haki wamekufa, wengine wana warithi, wengine bado wako hai na wengine hawajulikani walipo. Hivi sasa anatubu kwa majuto makubwa. Ni ipi njia ya kutoka katika viapo hivyo na madhara yake, huku akikhofia kuwa akiwafikishia wenye haki au warithi wao basi huenda yakazuka matatizo na madhara makubwa?

Jibu: Ni lazima arudishe haki zote kwa wenyewe. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kuwa na dhuluma kwa ndugu yake basi amwombe amsamehe leo kabla haijafika siku ambayo hakutakuwa na dinari wala dirhamu. Ikiwa ana mema, yatachukuliwa kwa kiwango cha dhuluma yake, na kama hana mema, atachukuliwa katika maovu yao na kubebeshwa yeye.”

Kwa hivyo ni wajibu wake kuwapa haki zao wale aliowadhulumu na kuapa juu ya kuzikana. Atubie kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa tawbah ya kweli na awaambie wazi kuwa alikosea na ametubu, kisha awarejeshee haki zao ikiwa wako hai.

Ama waliokufa, basi haki hizo wapewe warithi wao. Na wale waliopotea au wasiojulikana walipo, basi ajitahidi kuwatafuta kadiri ya uwezo wake. Iwapo hatoweza kabisa kuwafahamu au kuwafikia, basi atoe mali hiyo kama swadaqah kwa niaba yao kwa maskini na wahitaji. Ama kusema anyamazia suala hilo, hapana.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3158/حكم-من-حلف-على-عدم-رد-حقوق-الاخرين-وتاب-بعدها
  • Imechapishwa: 26/10/2026