Swali: Ikiwa baba amefariki na ana deni la swawm za Ramadhaan tatu – Je, nimfungie au nifanye nini?
Jibu: Ikiwa baba amefariki hali ya kuwa amefanya uzembe, ilihali Allaah alimpa afya na akapona maradhi, lakini akafanya uzembe, basi lililowekwa katika Shari´ah kwako ni kumfungia wewe pamoja na ndugu zako. Kwa sababu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote aliyekufa na ana deni la swawm, basi atafungiwa na walii wake.”
Walimuuliza watu kadhaa ambapo kila mmoja akisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Hakika baba yangu amefariki na ana deni fulani. Je, nimfungie?” Mwingine akasema: ”Mama yangu amefariki na ana deni fulani, je, nimfungie?” Mwingine akasema: ”Dada yangu amefariki na ana deni fulani, je, nimfungie?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
”Je, lau baba yako angekuwa na deni la mali, je, usingelilipa? Je, lau mama yako angekuwa na deni, usingelilipa?” Basi lipeni deni la Allaah, kwa sababu Allaah ndiye Mwenye haki zaidi kulipiwa.”
Hivyo ni juu yenu kulipa deni hilo kwa kumfungia wewe na ndugu zako. Hilo ni jambo lililowekwa katika Shari´ah kwenu, kwa maana ni Sunnah kwenu. Msipomfungia, basi mlisheni chakula masikini mmoja kwa kila siku kutoka katika mali yake. Hilo ni ikiwa hamkumfungia. Sunnah ni kumfungia baba yenu ikiwa alikuwa amepona maradhi yake kisha akafanya uzembe. Ama ikiwa alifariki akiwa bado katika maradhi yake na hakupata kupona, bali maradhi yaliendelea mpaka akafa, basi hakuna kulipa wala kulisha chakula.
Mwanafunzi: Yamedondoka kutoka kwake?
Ibn Baaz: Yamedondoka kutoka kwake kwa sababu alikuwa ni mwenye udhuru.
Mwanafunzi: Vipi kuhusu swalah?
Ibn Baaz: Swalah hailipwi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2849/حكم-الصيام-عن-الوالد-اذا-مات
- Imechapishwa: 21/02/2026
Swali: Ikiwa baba amefariki na ana deni la swawm za Ramadhaan tatu – Je, nimfungie au nifanye nini?
Jibu: Ikiwa baba amefariki hali ya kuwa amefanya uzembe, ilihali Allaah alimpa afya na akapona maradhi, lakini akafanya uzembe, basi lililowekwa katika Shari´ah kwako ni kumfungia wewe pamoja na ndugu zako. Kwa sababu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote aliyekufa na ana deni la swawm, basi atafungiwa na walii wake.”
Walimuuliza watu kadhaa ambapo kila mmoja akisema: ”Ee Mtume wa Allaah! Hakika baba yangu amefariki na ana deni fulani. Je, nimfungie?” Mwingine akasema: ”Mama yangu amefariki na ana deni fulani, je, nimfungie?” Mwingine akasema: ”Dada yangu amefariki na ana deni fulani, je, nimfungie?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
”Je, lau baba yako angekuwa na deni la mali, je, usingelilipa? Je, lau mama yako angekuwa na deni, usingelilipa?” Basi lipeni deni la Allaah, kwa sababu Allaah ndiye Mwenye haki zaidi kulipiwa.”
Hivyo ni juu yenu kulipa deni hilo kwa kumfungia wewe na ndugu zako. Hilo ni jambo lililowekwa katika Shari´ah kwenu, kwa maana ni Sunnah kwenu. Msipomfungia, basi mlisheni chakula masikini mmoja kwa kila siku kutoka katika mali yake. Hilo ni ikiwa hamkumfungia. Sunnah ni kumfungia baba yenu ikiwa alikuwa amepona maradhi yake kisha akafanya uzembe. Ama ikiwa alifariki akiwa bado katika maradhi yake na hakupata kupona, bali maradhi yaliendelea mpaka akafa, basi hakuna kulipa wala kulisha chakula.
Mwanafunzi: Yamedondoka kutoka kwake?
Ibn Baaz: Yamedondoka kutoka kwake kwa sababu alikuwa ni mwenye udhuru.
Mwanafunzi: Vipi kuhusu swalah?
Ibn Baaz: Swalah hailipwi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2849/حكم-الصيام-عن-الوالد-اذا-مات
Imechapishwa: 21/02/2026
https://firqatunnajia.com/amzazi-aliyefariki-huku-anadaiwa-baadhi-ya-siku-za-ramadhaan/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket