Swali: Niliweka nadhiri kwa Allaah kuwa nitafanya ´Aqiyqah ngamia ikiwa ataniruzuku mapacha. Je, baada ya hapo inabidi nichinje kitu kingine kwa ajili ya watoto hao wawili baada ya kuruzukiwa mapacha?

Jibu: Sunnah ni kuwachinjia kwenye ´Aqiyqah kondoo/mbuzi. Lakini kwa kuwa umeweka nadhiri, basi timiza nadhiri yako. Lakini Sunnah ni kondoo, si ngamia. Kwa kila mtoto wa kiume ni kondoo wawili, wawe ni wana-kondoo waliokomaa au mbuzi wa mwaka wa pili. Hii ndiyo Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameagiza kuchinjwa kondoo wawili kwa mtoto wa kiume na kondoo mmoja kwa mtoto wa kike. Ikiwa umeweka nadhiri pia ngamia kwa ajili ya Allaah, basi mchinje ngamia huyo, kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yeyote mwenye kuweka nadhiri ya kumtii Allaah, basi na amtii.

Swali: Je, ngamia anatosha badala ya kondoo?

Ibn Baaz: Hapana, haitoshi. Sunnah ni kondoo/mbuzi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30954/هل-يجزى-الجمل-في-العقيقة-لمن-نذره
  • Imechapishwa: 18/09/2025