Ametufu, kufanya Sa´y na kuswali ´iyd bila twahara

Swali: Nilikuja kufanya Twawaaf-ul-Ifaadhwah siku ya ´iyd ambapo nikaingia Haram pamoja na watu niliokuwa nao. Kabla ya kuingia nilikuwa na wudhuu´, lakini ukavunjika na kwa kutokujua sehemu ya kutawadhia nikawaonea aibu wale niliokuwa nao na sikutaka kuchelewa nao. Matokeo yake nikaswali swalah ya ´iyd, nikafanya Twawaaf, Sa´y na kuswali mahali aliposimama Ibraahiym bila ya wudhuu´?

Jibu: Unapaswa kurudia Twawaaf. Jitwaharisha kisha urudie Twawaaf kwa nia ya  hajj yako hii. Ama Sa´y inasihi, kwa sababu Sa´y haishurutishi kuwa na twahara. Lakini hakuna vibaya ukiirudia pamoja na Twawaaf. Kuhusu swalah uliyoiswali; ikiwa ni swalah ya ´iyd, basi jambo lake ni lenye wasaa kwa sababu ni faradhi ya kutoshelezana. Lakini ikiwa uliswali swalah ya faradhi kama Dhuhr au nyingine, basi urudie swalah hiyo. Ama ikiwa ni swalah ya ´iyd, basi si lazima kurudia. Lakini ukiirudia kwa kuchukua tahadhari, ni vizuri kwa sababu baadhi ya wanazuoni wamesema ni wajibu kwa kila mtu. Ukirudia pia Sa´y pamoja na Twawaaf, ni vyema. Vinginevyo Sa´y yako inatosha.

Swali: Je, aibu hii aliyopata inajuzu?

Jibu: Hapana, hii ni makosa na haijuzu. Ni wajibu usiswali wala kutufu isipokuwa ukiwa na twahara. Hii si haya ya kweli, bali ni udhaifu. Ni wajibu wako kumcha Allaah. Ikiwa huna wudhuu´ uharakishe kwenda kutawadha, hata kama utachelewa kufanya Twawaaf au kwa wenzako. Uende ukaulize ni wapi pa kutawadhia? Watu watakuonyesha, utawadha kisha ufanye Twawaaf pamoja na watu. Baada ya hapo, usirudie tena jambo hili, kwani ni jambo baya lisilojuzu.

Swali: Vipi kwa upande wa Sa´y?

Jibu: Sa´y ni nyepesi zaidi, lakini ikiwa inafanywa kwa twahara ni bora zaidi. Vinginevyo inatosha hata bila twahara, lakini kuwa na twahara ni bora na ni nzuri zaidi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3289/حكم-الطواف-والسعي-وصلاة-العيد-بدون-وضوء
  • Imechapishwa: 10/10/2026