Amemfanya tendo la ndoa na msichana baada ya ndoa lakini kabla ya kufanya walima

Swali: Kijana mmoja alifunga ndoa na msichana, lakini kabla ya ndoa kutangazwa hadharani alifanya naye tendo la ndoa. Je, hili ni haramu? Je, linachukuliwa kuwa ni dhambi?

Jibu: Si haramu, lakini bora ni kutofanya hivo mpaka ndoa itakapokamilika mradi mkataba wa ndoa umekwishafungwa na kuenea. Hakuna ubaya wowote. Lakini kinachotakiwa ni yeye kusubiri mpaka atakapomuweka ndani.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/206)
  • Imechapishwa: 20/02/2026