Swali: Kuna mtu ameweka kiasi cha fedha katika benki fulani kwa namna ya amana, bila ya kupata faida. Baadaye akagundua kuwa benki hiyo inafanya kazi na kuendesha miradi iliyo haramu.
Jibu: Inapaswa kulinda mali na kutoziweka katika benki zinazofanya ribaa kadiri inavyowezekana. Lakini akilazimika kufanya hivyo, akaweka fedha benkini kwa lengo la kuzihifadhi tu, bila kuridhia ribaa, bila kuitaka wala bila kuchukua faida yoyote, basi tunatarajia kuwa hana dhambi kwa sababu ya dharurah khaswa katika zama hizi. Kwa sababu baadhi ya watu wakihifadhi fedha majumbani mwao huogopa kuibiwa au kupoteza mali zao. Kwa kumalizia ni kwamba ikiwa dharurah imemlazimisha kuweka fedha benkini kwa ajili ya kuzihifadhi tu na hana nia ya kupata faida ya ribaa, basi hakuna dhambi juu yake.
Swali: Ni yepi maoni yenye nguvu?
Jibu: Maoni yenye nguvu hatujui kuwa na tatizo. Maoni yenye nguvu ni kwamba hakuna tatizo akiweka kwenye as-Subay‘iy na benki zinazofanana nazo. Hatujui chochote juu yake isipokuwa kheri tu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1374/حكم-ايداع-الاموال-في-البنوك-الربوية-بدون-اخذ-فاىدة
- Imechapishwa: 05/04/2026
Swali: Kuna mtu ameweka kiasi cha fedha katika benki fulani kwa namna ya amana, bila ya kupata faida. Baadaye akagundua kuwa benki hiyo inafanya kazi na kuendesha miradi iliyo haramu.
Jibu: Inapaswa kulinda mali na kutoziweka katika benki zinazofanya ribaa kadiri inavyowezekana. Lakini akilazimika kufanya hivyo, akaweka fedha benkini kwa lengo la kuzihifadhi tu, bila kuridhia ribaa, bila kuitaka wala bila kuchukua faida yoyote, basi tunatarajia kuwa hana dhambi kwa sababu ya dharurah khaswa katika zama hizi. Kwa sababu baadhi ya watu wakihifadhi fedha majumbani mwao huogopa kuibiwa au kupoteza mali zao. Kwa kumalizia ni kwamba ikiwa dharurah imemlazimisha kuweka fedha benkini kwa ajili ya kuzihifadhi tu na hana nia ya kupata faida ya ribaa, basi hakuna dhambi juu yake.
Swali: Ni yepi maoni yenye nguvu?
Jibu: Maoni yenye nguvu hatujui kuwa na tatizo. Maoni yenye nguvu ni kwamba hakuna tatizo akiweka kwenye as-Subay‘iy na benki zinazofanana nazo. Hatujui chochote juu yake isipokuwa kheri tu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1374/حكم-ايداع-الاموال-في-البنوك-الربوية-بدون-اخذ-فاىدة
Imechapishwa: 05/04/2026
https://firqatunnajia.com/amegundua-kuwa-benki-inatumia-pesa-zake-katika-miradi-ya-haramu/