Amedhania kuwa kumeshaswaliwa msikitini na akaswali mwenyewe

Swali: Kuna mtu alikuwa anafikiri kuwa kumeshaswaliwa ´Aswr msikitini ambapo akawa ameswali mwenyewe. Baada ya kumaliza kuswali akasikia jinsi kunaswaliwa ´Aswr msikitini. Afanye nini?

Jibu: Ameshaswali. Ni mwenye kupewa udhuru kwa sababu alidhania kuwa watu wameshaswali. Ameshatekeleza faradhi yake kutokana na vile alivyodhania kuwa ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (11) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-07-24_0.mp3
  • Imechapishwa: 07/06/2020