Swali: Tunaomba maana ya Aayah hii ambayo inawatatiza watu wengi:
يَمْحُو اللَّـهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ ۖ وَعِندَهُ أُمُّ الْكِتَابِ
“Allaah anafuta yale ayatakayo na anathibitisha na Kwake ndiko kuna Mama wa Kitabu.”[1]
Jibu: Wanazuoni wamezungumzia Aayah hii, wamebainisha maana yake na kwamba inahusu mambo mengi. Inahusu madhambi na mema. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hufuta anayoyataka katika madhambi na maovu na huacha anayoyataka kulingana na hali ya mja. Akimtii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kusimama imara juu ya amri Yake, basi Allaah humwandikia mema na humfutia maovu. Akitubu kwa Allaah, humfutia maovu. Kadhalika Allaah hufuta anayoyataka katika Shari´ah mbalimbali, huzibadilisha na huweka anayoyataka katika zama za Mtume aliotumwa na Allaah, kama vile Allaah alivyotuwekea mwanzo kuelekea Qiblah Yerusalemu, kisha akatuwekea kuelekea Ka´bah. Allaah hufuta anayoyataka na huweka katika Shari´ah mbalimbali, madhambi, amri na makatazo.
Baadhi yao wamesema vivyo hivyo baadhi ya makadirio yaliyofungamanishwa ambapo Allaah hufuta anayoyataka katika makadirio yaliyofungamanishwa na huweka. Ama makadirio ambayo hayana njia ya kubadilika, ambayo ujuzi wa Allaah umeshatangulia kwamba yatatokea, haya hayafutwi. Bali yanabaki thabiti. Mfano wa hayo ni kifo. Hakuna anayenusurika nacho. Haya ni makadirio yaliyotangulia kwamba lazima yatokee. Vilevile mfano mwingine ni uzee. Lazima utokee kwa aliyeandikiwa kuishi. Mwisho wake ni kufikia uzee. Imekuja katika Hadiyth:
”Hakuna ugonjwa isipokuwa una dawa isipokuwa uzee.”
Imekuja katika tamko jengine:
”Hakuna ugonjwa isipokuwa una dawa isipokuwa kifo.”
[1] 13:39
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3441/ما-معنى-يمحوا-الله-ما-يشاء-ويثبت-وعنده-ام-الكتاب
- Imechapishwa: 05/11/2026
Swali: Tunaomba maana ya Aayah hii ambayo inawatatiza watu wengi:
يَمْحُو اللَّـهُ مَا يَشَاءُ وَيُثْبِتُ ۖ وَعِندَهُ أُمُّ الْكِتَابِ
“Allaah anafuta yale ayatakayo na anathibitisha na Kwake ndiko kuna Mama wa Kitabu.”[1]
Jibu: Wanazuoni wamezungumzia Aayah hii, wamebainisha maana yake na kwamba inahusu mambo mengi. Inahusu madhambi na mema. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) hufuta anayoyataka katika madhambi na maovu na huacha anayoyataka kulingana na hali ya mja. Akimtii Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na kusimama imara juu ya amri Yake, basi Allaah humwandikia mema na humfutia maovu. Akitubu kwa Allaah, humfutia maovu. Kadhalika Allaah hufuta anayoyataka katika Shari´ah mbalimbali, huzibadilisha na huweka anayoyataka katika zama za Mtume aliotumwa na Allaah, kama vile Allaah alivyotuwekea mwanzo kuelekea Qiblah Yerusalemu, kisha akatuwekea kuelekea Ka´bah. Allaah hufuta anayoyataka na huweka katika Shari´ah mbalimbali, madhambi, amri na makatazo.
Baadhi yao wamesema vivyo hivyo baadhi ya makadirio yaliyofungamanishwa ambapo Allaah hufuta anayoyataka katika makadirio yaliyofungamanishwa na huweka. Ama makadirio ambayo hayana njia ya kubadilika, ambayo ujuzi wa Allaah umeshatangulia kwamba yatatokea, haya hayafutwi. Bali yanabaki thabiti. Mfano wa hayo ni kifo. Hakuna anayenusurika nacho. Haya ni makadirio yaliyotangulia kwamba lazima yatokee. Vilevile mfano mwingine ni uzee. Lazima utokee kwa aliyeandikiwa kuishi. Mwisho wake ni kufikia uzee. Imekuja katika Hadiyth:
”Hakuna ugonjwa isipokuwa una dawa isipokuwa uzee.”
Imekuja katika tamko jengine:
”Hakuna ugonjwa isipokuwa una dawa isipokuwa kifo.”
[1] 13:39
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3441/ما-معنى-يمحوا-الله-ما-يشاء-ويثبت-وعنده-ام-الكتاب
Imechapishwa: 05/11/2026
https://firqatunnajia.com/allaah-anafuta-na-kukiacha-akitakacho/