Swali: Je, inajuzu kufunga au kutoa swadaqah badala ya damu kwa njia ya kuchagua au kipaumbele ni damu?
Jibu: Hapana. Hadiy ya Tamattu´ na Qiraan ni lazima damu; swadaqah na mali haisihi katika jambo hilo. Ama yasiyo hayo, kama fidia ya aliyefanya makatazo, kama kufunika kichwa chake kwa makusudi au akatia manukato kwa makusudi, hapa anapewa uchaguzi kati ya kufunga siku tatu, kuchinja kondoo mmoja au kulisha chakula masikini sita. Anachagua ikiwa amefunika kichwa chake, amevaa kilichoshonwa kwa makusudi akiwa anakumbuka, akatia manukato, akakata kucha zake au akanyoa nywele zake. Basi mambo haya matano ndani yake kuna mojawapo ya mambo matatu:
1 – Kufunga siku tatu katika sehemu yoyote.
2 – Kulisha masikini sita, kila masikini nusu pishi´.
3 – Kuchinja kondoo mmoja katika Haram huko Makkah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2231/احكام-الهدي
- Imechapishwa: 05/03/2026
Swali: Je, inajuzu kufunga au kutoa swadaqah badala ya damu kwa njia ya kuchagua au kipaumbele ni damu?
Jibu: Hapana. Hadiy ya Tamattu´ na Qiraan ni lazima damu; swadaqah na mali haisihi katika jambo hilo. Ama yasiyo hayo, kama fidia ya aliyefanya makatazo, kama kufunika kichwa chake kwa makusudi au akatia manukato kwa makusudi, hapa anapewa uchaguzi kati ya kufunga siku tatu, kuchinja kondoo mmoja au kulisha chakula masikini sita. Anachagua ikiwa amefunika kichwa chake, amevaa kilichoshonwa kwa makusudi akiwa anakumbuka, akatia manukato, akakata kucha zake au akanyoa nywele zake. Basi mambo haya matano ndani yake kuna mojawapo ya mambo matatu:
1 – Kufunga siku tatu katika sehemu yoyote.
2 – Kulisha masikini sita, kila masikini nusu pishi´.
3 – Kuchinja kondoo mmoja katika Haram huko Makkah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2231/احكام-الهدي
Imechapishwa: 05/03/2026
https://firqatunnajia.com/aliyefanya-makatazo-matano-anapaswa-kufanya-moja-katika-mambo-matano/