74. Amri inashuka kisha inapanda kwa Allaah

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ

”Anaendesha mambo kutoka mbinguni mpaka ardhini, kisha inapanda Kwake katika siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu katika ile mnayoihesabu nyinyi.”[1]

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ

“Wanamuogopa Mola wao Aliye juu yao na wanafanya yale wanayoamrishwa.”[2]

MAELEZO

Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anaendesha amri miongoni mwa maamrisho Yake ya kilimwengu na ya kidini:

مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ

“… kutoka mbinguni mpaka ardhini… “

Amri inashuka ardhini kutokea kwa Allaah mbinguni. Kisha inapanda Kwake. Ni dalili inayofahamisha kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko juu ya mbingu, kwa sababu kushuka inakuwa kutokea kwa juu.

Alipotaja namna ambavyo viumbe wanamsujudia, akasema:

يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ

“Wanamuogopa Mola wao Aliye juu yao na wanafanya yale wanayoamrishwa.”[3]

Hapa kunathibitishwa kuwepo juu kwa Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 32:05

[2] 16:50

[3] 16:50

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 112
  • Imechapishwa: 20/08/2024