Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

أَأَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يَخْسِفَ بِكُمُ الْأَرْضَ فَإِذَا هِيَ تَمُورُ أَمْ أَمِنتُم مَّن فِي السَّمَاءِ أَن يُرْسِلَ عَلَيْكُمْ حَاصِبًا ۖ فَسَتَعْلَمُونَ كَيْفَ نَذِيرِ

“Je, mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokudidimizeni ardhini, tahamaki hiyo inatikisika? Au mnadhani mko katika amani na aliyeko juu mbinguni kwamba hatokutumieni tufani ya mawe basi mtajua vipi maonyo Yangu?”[1]

MAELEZO

Neno (السَّمَاء) lina maana mbili:

1 – Ujuu. Hivyo inakuwa Allaah yuko (فِي السَّمَاء), bi maana juu.

2 – Mbingu zilizoumbwa. Katika hali hiyo kinachomaanishwa ni kwamba Allaah yuko juu ya mbingu. Kama alivosema Allaah (Ta´ala):

وَلَأُصَلِّبَنَّكُمْ فِي جُذُوعِ النَّخْلِ

“Nitakusulubuni katika (فِي) mashina ya mitende.”[2]

Bi maana juu ya mashina ya mtende.

فَسِيحُوا فِي الْأَرْضِ

“Basi tembeeni katika (فِي) ardhi… ”[3]

Bi maana juu ya ardhi.

[1] 67:16-17

[2] 20:71

[3] 9:2

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 111
  • Imechapishwa: 19/08/2024