Kuhusu masimulizi ya Maswahabah na wanafunzi wa Maswahabah katika maneno na matendo yao ni mengi zaidi ya kuhesabika. Haya yote ni kwa yule asiyeogopa kujionyesha, kujivuna, mambo mengine mabaya na ambaye hawadhuru wengine kwa kuwachanganya katika swalah zao. Imenukuliwa kutoka kwa kundi la Salaf kuchagua kusoma kimyakimya kwa sababu ya khofu ya mambo yaliyotajwa. al-A´mash amesema:
”Niliingia kwa Ibraahiym akiwa anasoma ndani ya msahafu. Bwana mmoja akaomba idhini ya kuingia ambapo akaufunika na kusema: ”Asije akaona kuwa nasoma kila wakati.”
Abul-´Aaliyah amesema:
”Nilikuwa nimekaa na Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo mmoja wao akasema: ”Nilisoma usiku huu kiasi fulani cha Qur-aan.” Ndipo wakasema: ”Hiyo ndiyo sehemu yako uliyopata.”
Watu hawa wanajengea hoja kwamba ´Uqbah bin ´Aamir (Radhiya Allaahu ´anh) amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Anayesoma Qur-aan kwa sauti ya juu ni kama anayetoa swadaqah kwa wazi, na anayesoma kimyakimya ni kama anayetoa swadaqah kimyakimya.”[1]
Ameipokewa Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri, na an-Nasaa´iy.
at-Tirmidhiy amesema:
”Maana yake ni kwamba anayesoma Qur-aan kimyakimya ni bora kuliko anayesoma kwa sauti ya juu, kwa sababu kutoa swadaqah kwa siri ni bora kwa mtazamo wa wanazuoni kuliko kutoa swadaqah waziwazi. Wanazuoni wanaifahamu kwamba mtu asiingie katika jambo la kujiona. Kwa sababu anayefanya kitendo kwa siri haogopi kujivuna kama anavyoweza kuogopa akifanya hivo waziwazi.”[2]
Yote haya yanaenda sambamba na yale yaliyotangulia mwanzo wa sehemu hii ya ufafanuzi; kwamba ikiwa ataogopa jambo lisilopendeza kwa sababu ya kusoma kwa sauti ya juu basi asisome kwa sauti ya juu, na ikiwa haogopi basi inapendekezwa kusoma kwa sauti ya juu. Ikiwa kusoma ni kwa kundi lililokusanyika, basi inapendekezwa zaidi kusoma kwa sauti ya juu kwa sababu ya yale yaliyotangulia na kwa faida inayowafikia wengine – na Allaah ndiye Mjuzi zaidi.
[1] Abu Daawuud (1333), at-Tirmidhiy (2919), aliyesema kuwa ni nzuri, na an-Nasaa’iy (2561). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (1333).
[2] al-Jaamiy´(2919).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 67-68
- Imechapishwa: 24/11/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 67-68
Imechapishwa: 24/11/2026
https://firqatunnajia.com/65-kisomo-cha-kimyakimya-kinachopendeza/