Kuhusu masimulizi yaliyonakiliwa ni mengi na kwa ajili hiyo nitataja baadhi yake. Imethibiti ya kwamba Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
“Allaah hasikilizi kitu kama anavyomsikiliza Nabii mwenye sauti nzuri anayeisoma Qur-aan kwa kuipamba na kuinua sauti juu.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
Kusikiliza Kwake ni ishara ya ridhaa na kukubali.
Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:
“Hakika umepewa sauti nzuri miongoni mwa sauti nzuri za Daawuud.”[2]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim. Kwa Muslim imekuja ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:
“Jana usiku nilisikiliza kisomo chako.”
Hadiyth ameisimulia Buraydah bin al-Haswib.
Fudhwaalah bin ´Ubayd (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah anamsikiliza zaidi mtu mwenye sauti nzuri katika Qur-aan kuliko mwenye ala ya muziki anavyoisikiliza ala yake.”[3]
Ameipokea Ibn Maajah.
Abu Muusa al-Ash´ariy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia pia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ninazitambua sauti za kundi la al-Ash´ar usiku unapoingia. Ninatambua makazi yao kwa sauti zao za Qur-aan usiku, hata kama sikuwaona waliposhuka mchana.”[4]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
al-Baraa´ bin ´Aazib (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Pambeni Qur-aan kwa sauti zenu.”[5]
Ameipokea Abu Daawuud, an-Nasaa’iy na wengineo.
Ibn Abiy Daawuud amepokea:
”´Aliy bin Abiy Twaalib alisikia kelele za watu msikitini wakisoma Qur-aan, ambapo akasema: “Twubaa kwa watu hawa! Walikuwa ndio watu waliopendwa zaidi kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[6]
Kuna Hadiyth nyingi zinazothibitisha kusoma kwa sauti ya juu.
[1] al-Bukhaariy (5023-5024) na Muslim (792).
[2] al-Bukhaariy (5048) na Muslim (793).
[3] Ibn Maajah (1340). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Ibn Maajah” (250).
[4] al-Bukhaariy (4232) na Muslim (2499).
[5] Abu Daawuud (1468), an-Nasaa’iy (1015-1016) na Ibn Maajah (1342). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (1468).
[6] al-Haythamiy amesema:
“Katika cheni ya wapokezi kuna Hafsw bin Sulaymaan al-Ghaadhiriy, ambaye ni mwenye kuachwa.” (Majma´-uz-Zawaa-id (7/169))
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 66-67
- Imechapishwa: 23/11/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 66-67
Imechapishwa: 23/11/2026
https://firqatunnajia.com/64-kisomo-cha-sauti-ya-juu-kinachopendeza/