Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Wamekubali viwango vyao walivyoandika katika vitabu vyao. Mmoja katika wakuu wao amesema:

Mwisho wa akili ni kamba 

Jitihada za viumbe wengi ni bure 

Roho zetu zimetelekezwa kwenye viwiliwili vyetu 

Mwisho wa dunia yetu ni mabalaa na adhabu 

Wakati wa uhai wetu wote hatukufaidika lolote katika utafiti wetu 

Isipokuwa tumekusanya yaliyosemwa 

Baada ya hapo akasema:

“Nimetafakari mifumo inayofuatwa na wanafalsafa na kuona kuwa haifidishi lolote. Nimekuta mfumo wa karibu zaidi ni mfumo wa Qur-aan. Soma kuhusu kuthibitisha:

الرَّحْمَنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَى

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[1]

إِلَيْهِ يَصْعَدُ الْكَلِمُ الطَّيِّبُ وَالْعَمَلُ الصَّالِحُ يَرْفَعُهُ

“Kwake Yeye linapanda neno zuri na kitendo chema hukinyanyua.”[2]

Soma kuhusu kukanusha:

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”[3]

وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا

“Na wala wao hawawezi kuzunguka elimu Yake.”

Mwenye kukutana na niliyokutana nayo, basi atajua niliyoyajua.”[4]

MAELEZO

Baadhi yao wamesema wazi mikanganyiko na vurugu zao. Hii ndio hoja dhidi yao. Aliyesema hayo hapo juu ni miongoni mwa vigogo vyao; al-Fakhr ar-Raaziy, mtunzi wa ”at-Tafsiyr al-Kabiyr”. Mwishoni mwa uhai wake alijirejea kutokana na ´Aqiydah yake na akatubu kwa Allaah (´Azza wa Jall), kama inavotajwa katika beti hizi. Amekubali mwenyewe kuwa akili zimesimama na imeshindwa kuifikia haki. Wafikiriaji wamekata tamaa kwa sababu wameshika njia yenye giza. Wamechoka juu ya utafiti wa muda mrefu ambao haukupelekea katika matokeo yoyote. Utaona vitabu vya wanafalsafa vimejaa nukuu kutoka kwa watu na makinzano yasiyokuwa na mwisho. Hawanukuu Qur-aan na Sunnah. Vitabu vyao vimejaa mijadala tu, kuhusu vitabu vya ´Aqiydah vya Ahl-us-Sunnah vimejengeka juu yale aliyosema Allaah, yale aliyosema Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na yale yaliyosemwa na Salaf.

[1] 20:5

[2] 35:10

[3] 42:11

[4] Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (5/11).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 90-91
  • Imechapishwa: 12/08/2024