45. Nyimbo ya wabebaji wa ´Arshi

42 – Hassaan bin ´Atwiyyah amesema:

”Wabebaji wanane wa ´Arshi wanaimba kwa sauti nzuri na za kupendeza. Wanne katika wao husema: ”Kutakasika kutokana na mapungufu ni Kwako. Himdi zote njema ni Zako kwa upole na ujuzi Wako.” Wanne wengine husema: ”Kutakasika kutokana na mapungufu ni Kwako. Himdi zote njema ni Zako kwa msamaha Wako baada ya uwezo Wako.”[1]

Cheni ya wapokezi ni yenye nguvu.

[1] Mtunzi wa kitabu ameitaja kupitia kwa al-Waliyd bin Yaziyd al-´Adhriy: al-Awzaa´iy ametuhadithia, kutoka kwake. Cheni hii ya wapokezi ni yenye nguvu, kama alivosema. Rawaad bin al-Jarraah ameisimulia kupitia kwa al-Awzaa´iy. Ameipookea Abush-Shaykh katika “al-´Adhwamah” (1/88 – muswada).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk 101
  • Imechapishwa: 24/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy