40. Vitabu vinavyokufunza ´Aqiydah ya Salaf

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Wala muislamu hawezi kuamini kwamba walikuwa ni wenye kuitakidi kimakosa. Mtu mwenye busara ambaye anatambua hali ya watu hao hawezi kufikiria kitu kama hicho. Isitoshe wana maneno mengi muhimu ambayo hayawezi kupata nafasi katika fatwa hii. Anajua hayo kila yule ambaye anayafuatilia.

MAELEZO

Walizisoma Aayah na Hadiyth zinazozungumzia majina na sifa, lakini hawakuamini kuwa zinafahamisha jambo kama wanavoona Jahmiyyah na vifaranga vyao. Huu ni ukafiri na upotofu mkubwa, kwa sababu amewatuhumu viumbe bora na wao ndio karne bora ima kwa ujinga au kwamba waliitambua haki lakini hawakuiamini na badala yake wakaonelea kinyume chake. Mtazamo huu ni upotofu mkubwa. Yule ambaye anawajua Maswahabah, wanafunzi wa Maswahabah na wanafunzi wa wanafunzi wa Maswahabah na maisha yao na kujitahidi kwao katika kuitafuta elimu na katika ´ibaadah na kwamba waliyatumia maisha yao mazima katika mambo hayo ataona kuwa walitilia mkazo zaidi maudhui haya kushinda namna walivyotilia mkazo mambo mengine na kwamba hilo ndilo jambo lilikuwa na umuhimu zaidi kwao.

Salaf walizungumzia sana majina na sifa za Allaah, ´Aqiydah na Tawhiyd. Maneno yao hayawezi kupata nafasi katika fatwa hii. Hata hivyo unaweza kuyapata katika vitabu vikubwa kama vile ”Kitaab-ut-Tawhiyd”, ”Kitaab-us-Sunnah”, ”Kitaab-ul-Iymaan” na ”Kitaab-ush-Shariy´ah”. Mapokezi yao yanatambulika na yameingia kwa ndani zaidi, yamesimuliwa kwa wingi katika vitabu kama ”Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah” ya al-Laalakaa’iy, ”Kitaab-us-Sunnah” ya ´Abdullaah bin Ahmad, ”Kitaab-us-Sunnah” ya al-Khallaal, ”Kitaab-ush-Shariy´ah” ya al-Aajurriy, ”Kitaab-ut-Tawhiyd” ya Ibn Khuzaymah na ”Kitaab-ut-Tawhiyd” ya Ibn Mandah. Vitabu hivi vimeandikwa na ni vingi. Katika fatwa hii Shaykh (Rahimahu Allaah) ametaja kitu kidogo tu kuhusu wao kama mfano.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 72-73
  • Imechapishwa: 05/08/2024