39. Baada ya kuhajiri watu waligawanyika mafungu mangapi?

Swali 39: Baada ya kuhajiri watu waligawanyika mafungu mangapi?

Jibu: Makkah ilikuwa kati ya kafiri anayepiga vita Uislamu na muumini mnyonge asiyeweza kuhama. Madiynah ilikuwa kati ya muumini anayependa na kuchukia kwa ajili ya Allaah, ambao ni Wahajiri na Wanusuraji, mayahudi na wanafiki. Pindi watu hawa wanapokutana na waumini, husema: ”Tumeamini”; lakini wanapokuwa wao peke yao na mashaytwaan wao, husema: ”Hakika sisi tuko pamoja nanyi.”

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnjia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 107
  • Imechapishwa: 05/10/2023