37. Kisomo cha Qur-aan katika ´Ishaa’

5- ´Ishaa’

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma Suurah za Mufasswal za kati na kati katika zile Rak´ah mbili za mwanzo[1].

Wakati mwingine alikuwa akisoma “ash-Shams” na Suurah mfano wake[2].

Mara nyingine inatokea (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasoma Suurah “al-Inshiqaaq” na akileta Sujuud kwayo[3].

Kuna siku moja alisoma safarini Suurah “at-Tiyn” katika Rak´ah ya kwanza[4].

Amekataza mtu kurefusha kisomo katika ´Ishaa’. Mu´aadh alikuwa akiwaswalisha marafiki zake ´Ishaa’ na akirefusha kisomo. Hivyo akatoka mwanaume mmoja katika Answaar nje ya swalah na akaswali kivyake. Pindi Mu´aadh alipopewa khabari ya aliyoyafanya akasema: “Ni mnafiki.” Pindi yalipomfikia hayo mtu yule akaenda moja kwa moja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumweleza aliyoyasema Mu´aadh. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema kumwambi:

“Ee Mu´aadh! Hivi wewe unataka kuwa mfitini mkubwa?” Unapowaongoza watu katika swalah basi soma “ash-Shams”, “al-Layl”, “al-´Alaq” na “al-Layl”. Kuna wazee, watu wadhaifu na watu wenye haja wanaoswali nyuma yako.”[5]

[1] an-Nasaa’iy na Ahmad kwa mlolongo wa wapokezi Swahiyh.

[2] Ahmad na at-Tirmidhiy ambaye amesema ni nzuri.

[3] al-Bukhaariy, Muslim naa an-Nasaa’iy.

[4] al-Bukhaariy, Muslim naa an-Nasaa’iy.

[5] al-Bukhaariy, Muslim na an-Nasaa’iy na imetajwa katika ”al-Irwaa’” (295).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 101-102
  • Imechapishwa: 06/02/2017