Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye [washirika] na hali ya kuwa nyinyi mnajua [kuwa hana].” (02:22)

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ

”Na miongoni mwa watu wako waaowafanya badala ya Allaah kuwa ni mungu mshirika ambapo wanawapenda kama mapenzi [yapasavyo] ya kumpenda Allaah.” (02:165)

MAELEZO

Aayah zote hizi ni zenye kubainisha baadhi ya sifa za Allaah (´Azza wa Jall) kama zile zilizotangulia. Mfumo wa Ahl-us-Sunnah kwazo inatakiwa kuziamini na kuzithibitisha kama zilivyokuja kwa njia inayolingana na Allaah. Inatakiwa kufanya hivyo pasi na upotoshaji, ukanushaji, kuzifanyia namna wala kuzifananisha.

Hali kadhalika inahusiana na zile sifa za Allaah zilizokuja katika Sunnah Swahiyh. Zote ni kwa mfumo huu: ni wajibu kumthibitishia nazo Allaah kwa njia inayolingana na Allaah pasi na upotoshaji, ukanushaji, kuzifanyia namna wala kuzifananisha. Miongoni mwazo ni maneno Yake (Jalla wa ´Alaa):

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye [washirika] na hali ya kuwa nyinyi mnajua [kuwa hana].”

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا

”Na miongoni mwa watu wako waaowafanya badala ya Allaah kuwa ni mungu mshirika.”

Bi maana wenza na washirika. Allaah hana wenza wala washirika. Maneno Yake:

وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا

”Na miongoni mwa watu wako waaowafanya badala ya Allaah kuwa ni mungu mshirika.”

kwa njia ya makemeo. Kwa msemo mwingine kuna watu wenye kumfanyia Allaah washirika. Nao si wengine ni washirikina. Ndipo akakataza hili pale aliposema:

فَلَا تَجْعَلُوا لِلَّـهِ أَندَادًا وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ

“Basi msimfanyie Allaah waliolingana naye [washirika] na hali ya kuwa nyinyi mnajua [kuwa hana].”

Bi maana msiwaabudu waliyomo ndani ya makaburi, Mitume, Malaika, majini na mawe. Vyote hivyo kuviabudu ni batili. Amesema (Ta´ala):

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ هُوَ الْبَاطِلُ

“Hivyo ni kwa kuwa Allaah ndiye wa Haki na wale wanaowaomba badala Yake ndiyo batili.” (22:62)

ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّـهَ هُوَ الْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ الْبَاطِلُ

“Hivyo ni kwa kuwa Allaah ndiye wa Haki na wale wanaowaomba badala Yake ni batili.” (31:30)

Ni wajibu kwa kila kiumbe ambaye ´ibaadah ni yenye kumuwajibikia kumuabudu Yeye Mmoja pekee na wawakanushe wenza. Wanatakiwa kutambua kwa yakini ya kwamba hana mwenza, mwenye kulinhgana Naye na mshirika na wakati huohuo waamini hilo. Amesema (Ta´ala):

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

”Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala haiwi awe na yeyote anayefanana kulingana Naye.”

فَلَا تَضْرِبُوا لِلَّـهِ الْأَمْثَالَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ

”Basi msipigie mifano Allaah! Hakika Allaah Anajua nanyi hamjui.”

لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ

“Hakuna chochote kinachofanana Naye – Naye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waaswitwiyyah, uk. 39-41
  • Imechapishwa: 21/10/2024