25. Adhkaar baada ya kumaliza kuswali

66-

أَسْـتَغْفِرُ الله، أَسْـتَغْفِرُ الله، أَسْـتَغْفِرُ الله، اللّهُـمَّ أَنْـتَ السَّلامُ، وَمِـنْكَ السَّلام، تَبارَكْتَ يا ذا الجَـلالِ وَالإِكْـرام

”Namuomba Allaah msamaha, namuomba Allaah msamaha,  namuomba Allaah msamaha. Ee Allaah! Wewe ndiye as-Salaam na amani inatoka Kwako na umetukuka, Ee Mwenye utukufu na ukarimu.”[1]

67-

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْد، وهوَ على كلّ شَيءٍ قَدير، اللّهُـمَّ لا مانِعَ لِما أَعْطَـيْت، وَلا مُعْطِـيَ لِما مَنَـعْت، وَلا يَنْفَـعُ ذا الجَـدِّ مِنْـكَ الجَـد

”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake na himdi zote njema ni Zake na Yeye juu ya kila jambo ni muweza.  Ee Allaah! Hakuna awezaye kuzuia ulichokitoa na wala kutoa ulichokizuia na wala utajiri wa mtu haumnufaishi mwenye utajiri mbele Yako.”[2]

68-

لا إلهَ إلاّ اللّه وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمد، وهوَ على كلّ شيءٍ قدير، لا حَـوْلَ وَلا قـوَّةَ إِلاّ بِاللهِ، لا إلهَ إلاّ اللّـه، وَلا نَعْـبُـدُ إِلاّ إيّـاه، لَهُ النِّعْـمَةُ وَلَهُ الفَضْل وَلَهُ الثَّـناءُ الحَـسَن، لا إلهَ إلاّ اللّهُ مخْلِصـينَ لَـهُ الدِّينَ وَلَوْ كَـرِهَ الكـافِرون

”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake na himdi zote njema ni Zake na Yeye juu ya kila jambo ni muweza.  Hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, wala hatumwabudu mwengine isipokuwa Yeye, ni Zake neema, fadhilah ni Zake na ni Zake sifa zote nzuri, hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kumtakasia Yeye dini, ijapokuwa watachukia makafiri.”[3]

69-

سُـبْحانَ الله

”Allaah ametakasika kutokamana na mapungufu.”

 mara 33.

الحَمْـدُ لله

”Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

mara 33.

واللهُ أكْـبَر

”Allaah ni mkubwa.”

mara 33.

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحْـدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمْد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَـدير

”Hapana mungu wa haki isipokuwa ni Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika. Ufalme ni Wake na himdi zote njema ni Zake na Naye juu ya kila jambo ni muweza.”[4]

70-

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم. قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ اللَّـهُ الصَّمَدُ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu. Sema: ”Allaah ni Mmoja pekee, Mwenye kutegemewa kwa haja zote, hakuzaa na wala hakuzaliwa na wala haiwi awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye.”[5]

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ .قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَق مِن شَرِّ مَا خَلَقَ وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ  وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu. Sema: ”Najilinda na Mola wa mapambazuko, kutokamana na shari ya alivyoviumba, na kutokamana na shari ya giza linapoingia, kutokamana na shari ya wapulizao mafundoni na kutokamana na shari ya hasidi anapohusudu.”[6]

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ .قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ مَلِكِ النَّاسِ إِلَـٰهِ النَّاسِ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu. Sema: ”Najilinda na Mola wa watu, mfalme wa watu, mwabudiwa wa haki wa watu, kutokamana na shari za anayetia wasiwasi, mwenye kurejea nyuma, anayetia wasiwasi nyoyoni mwa watu miongoni mwa majini na watu.”[7]

Baada ya swalah zote[8].

71-

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ

”Allaah, hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye, Aliyehai daima, Mwenye kusimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anaombea mbele Yake bila ya idhini Yake? Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawakizunguki chochote katika elimu Yake isipokuwa kwa akitakacho. Kursiy Yake imeenea mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye yujuu kabisa, Ametukuka.”[9]

Baada ya swalah zote[10].

72-

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ المُلكُ ولهُ الحَمْد، يُحيـي وَيُمـيتُ وهُوَ على كُلّ شيءٍ قدير

“Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana mshirika, ufalme ni Wake, himdi zote njema ni Zake, anahuisha, anafisha na Yeye juu ya kila jambo ni muweza.”

Mara kumi baada ya swalah ya Maghrib na Fajr[11].

73-

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ عِلْمـاً نافِعـاً، وَرِزْقـاً طَيِّـباً، وَعَمَـلاً مُتَقَـبَّلاً

”Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba elimu yenye kunufaisha, riziki nzuri na matendo yanayotakabaliwa.”

Baada ya kutoa salamu ya swalah ya Fajr[12].

[1] Muslim (01/414) kwa nambari (591).

[2] al-Bukhaariy (01/255) kwa namnari (844), Muslim (01/414) kwa nambari (593).

[3] Muslim (01/415) kwa nambari (594).

[4] Muslim (01/418) kwa nambari (597) na ndani yake amesema:

”Yule mwenye kusema hivo baada ya kila swalah basi atasamehewa makosa yake ingawa ni mfano wa povu la bahari.”

[5] 112:01-04

[6] 113:01-05

[7] 114:01-06

[8] Abu Daawuud (02/86) kwa nambari (1523), at-Tirmidhiy (2903), an-Nasaa´iy (03/68) kwa nambari (1335). Tazama “Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (02/08). Suurah tatu hizo huitwa ”Mu´awwidhaat”. Tazama ”Fath-ul-Baariy” (09/62).

[9] 02:255

[10] Atakayeisoma baada ya kila swalah hakuna kitachomzuia kuingia Peponi isipokuwa kifo tu. Ameipokea an-Nasaa´iy katika ”´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (100), Ibn Sunniy (121). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy” (05/339), Silsilah Ahaadiyth-is-Swahiyhah” (02/697) kwa nambari (972).

[11] at-Tirmidhiy (05/515) kwa nambari (3474), Ahmad (04/227) kwa nambari (17990) ambaye ameifanya kuwa nzuri kupitia zengine ”al-Musnad” iliyohakikiwa (29/512). Tazama upokezi wake katika ”Zaad-ul-Ma´aad” (01/300).

[12] Ibn Maajah kwa nambari (925), an-Nasaa´iy katika ”´Amal-ul-Yawm wal-Laylah” (102). Tazama ”Swahiyh Ibn Maajah” (01/152), ”Majma´-uz-Zawaaid” (10/111). Itakuja kwa nambari. (95).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 22/02/2020