Jahmiyyah na Jabriyyah ni wafuasi wa Jahm bin Swafwaan at-Tirmidhiy. ´Aqiydah yake aliichukua kutoka kwa myahudi kwa jina Twaaluut, ambaye na yeye aliichukua kutoka kwa Lubayb bin al-Aswam, ambaye ndiye alimfanyia uchawi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kipote hichi ndicho kinachotetea ´Aqiydah inayosema kuwa Qur-aan imeumbwa. Aidha wanaamini pia kutenzwa nguvu, ambayo maana yake ni kwamba mja ametenzwa nguvu kwa matendo yake. Ndio maana wakanasibishwa kwa Jahm na wakaitwa Jahmiyyah. Jahm aliichukua kutoka kwa al-Ja´d, ambaye alikuwa akiishi mwishoni mwa dola ya Banuu Umayyah, na baadaye akauliwa na Khaalid bin ´Abdillaah al-Qasriy.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 265-266
  • Imechapishwa: 27/05/2025