19. Adabu za kutembea kwenda msikitini

Inapendekezwa kutembea kwenda kwenye swalah kwa utulivu na unyenyekevu, akurubishe hatua zake na wala asiunganishe vidole vyake. Aseme:

ٱلَّذِى خَلَقَنِى فَهُوَ يَهْدِينِ وَٱلَّذِى هُوَ يُطْعِمُنِى وَيَسْقِينِ وَإِذَا مَرِضْتُ فَهُوَ يَشْفِينِ وَٱلَّذِى يُمِيتُنِى ثُمَّ يُحْيِينِ وَٱلَّذِىٓ أَطْمَعُ أَن يَغْفِرَ لِى خَطِيٓـَٔتِى يَوْمَ ٱلدِّينِ رَبِّ هَبْ لِى حُكْمًۭا وَأَلْحِقْنِى بِٱلصَّـٰلِحِينَ وَٱجْعَل لِّى لِسَانَ صِدْقٍۢ فِى ٱلْـَٔاخِرِينَ وَٱجْعَلْنِى مِن وَرَثَةِ جَنَّةِ ٱلنَّعِيمِ وَٱغْفِرْ لِأَبِىٓ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلضَّآلِّينَ وَلَا تُخْزِنِى يَوْمَ يُبْعَثُونَ يَوْمَ لَا يَنفَعُ مَالٌۭ وَلَا بَنُونَ إِلَّا مَنْ أَتَى ٱللَّهَ بِقَلْبٍۢ سَلِيمٍۢ

“Ambaye Ameniumba, Naye  Huniongoza, na Ambaye ndiye Anayenilisha na  Kuninywesha. Na ninapokuwa mgonjwa, basi Yeye Huniponyesha. Na Ambaye Atanifisha kisha Atanihuisha. Na Ambaye natumai Atanisamehe makosa yangu Siku ya Malipo! Mola wangu! Nitunukie hukumu na Unikutanishe na waja wema; na Nifanye kusifika kwa heshima kwa vizazi watakaokuja baadaye. Na Nifanye miongoni mwa warithi wa mabustani ya Neema. Na Msamehe baba yangu – hakika yeye amekuwa miongoni mwa waliopotea. Na wala Usinihizi Siku watakayofufuliwa. Siku hayatofaa mali wala watoto, isipokuwa yule atakayemfikia Allaah na moyo uliosalimika.”[1]

Kisha aseme:

اللهم إني أسألك بحق السائلين عليك، وبحق ممشاي، فإني لم أخرج أشراً ولا بطراً ولا رياء ولا سمعة، خرجت اتقاء سخطك وابتغاء مرضاتك، أسألك أن تنقذني من النار، وأن تغفر لي ذنوبي، إنه لا يغفر الذنوب إلا أنت

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba kwa haki ya wale wenye kukuomba na kwa haki ya mwendo wangu huu. Hakika mimi sikutoka kwa kujivuna, wala kwa kiburi, wala kwa kujionyesha, wala kwa kutaka kusikika. Nimetoka kwa kuogopa ghadhabu Yako na kutafuta radhi Zako. Nakuomba Uniokoe na Moto na Unisamehe madhambi yangu. Hakika hakuna mwengine anayesamehe madhambi isipokuwa Wewe.”[2]

Ikiwa atasikia kunakimiwa swalah, basi asikimbilie. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalah inapokimiwa, msiende mkiwa mnakimbia. Bali iendeeni mkiwa na utulivu. Kile mtachowahi, basi kiswalini, na kile kitachokupiteni, basi kikamilisheni.”[3]

Swalah inapokimiwa, basi hakuna swalah nyingine isipokuwa ile swalah ya faradhi.

Anapofika msikitini, basi atatanguliza mguu wake wa kulia kuingia na aseme:

بسم الله، و الصلاة و السلام على رسول الله، اللهم اغفر لي ذنوبي، و افتح لي أبواب رحمتك

“Kwa jina la Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah. Ee Allaah! Nisamehe na Unifungulie milango ya rehema Zako.”

Anapotoka, basi atatanguliza mguu wake wa kushoto na aseme:

بسم الله، و الصلاة و السلام على رسول الله، اللهم اغفر لي ذنوبي، و افتح لي أبواب فَضْلِكَ

“Kwa jina la Allaah. Swalah na amani zimwendee Mtume wa Allaah. Ee Allaah! Nisamehe na Unifungulie milango ya fadhilah Zako.”

[1] 26:78-89

[2] Ahmad (11156) na Ibn Maajah (778). Dhaifu kwa maafikiano kwa mujibu wa Ibn Taymiyyah katika ”at-Tawassul wal-Wasiylah”, uk. 215.

[3] al-Bukhaariy (636) na Muslim (602).

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 23-24
  • Imechapishwa: 10/10/2026