Swali 18: Baadhi ya watu wanafikiri kuwa kukusanya na kufupisha ni mambo mawili yanayopasa kwenda sambamba; hakuna kukusanya pasi na kufupisha wala hakuna kufupisha pasi na kukusanya. Ni yepi maoni yenu juu ya hayo? Je, bora kwa msafiri ni kufupisha bila kukusanya au kukusanya na kufupisha[1]?
Jibu: Ambaye Allaah amemsunishia kufupisha, naye ni yule msafiri, basi itafaa kwake vilevile kukusanya. Bali hakuna uwiano kati ya mambo hayo mawili. Inafaa kwake kufupisha na wala asikusanye. Mtu akiwa ameshatua na si mwenye kuendelea na safari basi msafiri kuacha kukusanya ndio bora zaidi. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Minaa katika hajj ya kuaga. Alifupisha na wala hakukusanya. Katika vita vya Tabuuk aliunganisha kati ya kufupisha na kukusanya. Kwa hiyo ikajulisha kuna uwigo katika jambo hilo. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifupisha na akijumuisha pale anapokuwa bado yuko njiani anasafiri na si mwenye kutulizana mahali pamoja. Kuhusu kukusanya wigo wake ni mpana. Ni jambo linalofaa kwa wagonjwa na inafaa pia kwa waislamu katika misikiti wakati wa kunyesha mvua wakakusanya Maghrib na ´Ishaa, Dhuhr na ´Aswr. Lakini haijuzu kwao kufupisha. Kwa sababu kufupisha ni jambo maalum wakati wa safari peke yake.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/289-290).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 34-35
- Imechapishwa: 02/03/2022
Swali 18: Baadhi ya watu wanafikiri kuwa kukusanya na kufupisha ni mambo mawili yanayopasa kwenda sambamba; hakuna kukusanya pasi na kufupisha wala hakuna kufupisha pasi na kukusanya. Ni yepi maoni yenu juu ya hayo? Je, bora kwa msafiri ni kufupisha bila kukusanya au kukusanya na kufupisha[1]?
Jibu: Ambaye Allaah amemsunishia kufupisha, naye ni yule msafiri, basi itafaa kwake vilevile kukusanya. Bali hakuna uwiano kati ya mambo hayo mawili. Inafaa kwake kufupisha na wala asikusanye. Mtu akiwa ameshatua na si mwenye kuendelea na safari basi msafiri kuacha kukusanya ndio bora zaidi. Hivo ndivo alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Minaa katika hajj ya kuaga. Alifupisha na wala hakukusanya. Katika vita vya Tabuuk aliunganisha kati ya kufupisha na kukusanya. Kwa hiyo ikajulisha kuna uwigo katika jambo hilo. Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akifupisha na akijumuisha pale anapokuwa bado yuko njiani anasafiri na si mwenye kutulizana mahali pamoja. Kuhusu kukusanya wigo wake ni mpana. Ni jambo linalofaa kwa wagonjwa na inafaa pia kwa waislamu katika misikiti wakati wa kunyesha mvua wakakusanya Maghrib na ´Ishaa, Dhuhr na ´Aswr. Lakini haijuzu kwao kufupisha. Kwa sababu kufupisha ni jambo maalum wakati wa safari peke yake.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (10/289-290).
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 34-35
Imechapishwa: 02/03/2022
https://firqatunnajia.com/18-bora-kufupisha-na-kutokukusanya-kwa-msafiri-aliyetua/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)