16. Wanawafanyia maskhara Salafiyyuun kwa sababu wanakhalifu mwelekeo wao

16- Wafuasi wa mfumo wa al-Ikhwaan al-Muslimuun wanawafanyia maskhara wanachuoni wa Salafiyyah na wanafunzi wao wanaoenda kinyume na mwelekeo wao na kuwatuhumu kwamba ni “wanachuoni wa makaratasi”, “wanachuoni waovu” na “wakaaji”. Wakati huo huo wanatakasa ukaaji wao kwa maneno matupu kwa njia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) miaka kumi na tatu alilingania Makkah katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na kwamba hivi sasa sio wakati wa mapambano.

Ikiwa una shaka juu ya haya yaliyosemwa basi soma yale aliyoandika mwanaharakati mdogo[1] (ambaye kwa kiasi kikubwa amelelewa na vitabu vilivyoandikwa na wanadharia wa al-Ikhwaan al-Muslimuun). Sikiliza namna anavyowazungumzisha wanachuoni wa zama zote ambao wamejishughulisha na kuandika juu ya elimu ya Kishari´ah, kusimamisha nembo zote za Kiislamu na kulingania katika mfumo wa Salaf. Licha ya kwamba hawakufuata njia ile ile ya wanaharakati wanasiasa na wala hawakufanya uasi na mapinduzi dhidi ya watawala, amewazungumzisha ifuatavyo:

Swali na ufunge upendavyo

dini haimtambui mfanya ´ibaadah kupitia swalah na dini

Iache Tasbihi yako iwe ndefu kwa mita mbili,

vaa kilemba na kipake rangi

Wewe ni mmoja katika watawa wa mapadiri

Wewe sio katika dini ya Ahmad…

Ndugu mmoja katika wanachuoni watukufu akasema:

“Shairi hili linaita katika siasa potofu na iliyopinda na linawatweza wanachuoni, elimu yao na vitabu vyao. Kwa mujibu wake elimu yao haiwafai kitu na wala hawanufaiki kitu kwa swalah zao wala ´ibaadah zao midhali hawajishughulishi na uelewa wa kiharakati uliyozuliwa. Bali anawakufurisha kabisa pale aliposema:

Wewe ni mmoja katika watawa wa mapadiri

Wewe sio katika dini ya Ahmad.

Mtu mwenye shairi hili anaeneza vitabu ambavyo mwandishi wavyo ana makosa chungunzima na Bid´ah zisizojulikana. Baadhi ya waandishi hao ni Sayyid Qutwub na Abul-´Alaa´ al-Mawduudiy. Allaah awafanye wale wanaowafosi watu hawa kurudi katika haki[2].

[1] ´Aa’idh al-Qarniy.

[2] Imaam Swaalih al-Fawzaan amesema:

“Kijitabu hichi kilichoko mbele yetu kimeandikwa na ndugu yetu Shaykh Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy. Kinatahadharisha mifumo hii, kinabainisha athari zake mbaya na kinahimiza kushikamana barabara na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Allaah amjaze kheri na anufaishe kwa nasaha na maelekezo yake.” (Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 7)

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Asbaab Istiqaamat-ish-Shabaab wa Bawaa´ith Inhiraafihim, uk. 22
  • Imechapishwa: 25/03/2017