3 – Upokezi wa Yahyaa bin Yahyaa at-Tamiymiy[1]

al-Bayhaqiy amesema: Abu Bakr Ahmad bin Muhammad bin al-Haarith al-Faqiyh al-Aswfahaaniy[2] ametukhabarisha: Abu Muhammad ´Abdullaah bin Muhammad bin Ja’far bin Hayyaan[3], ambaye pia anatambulika kama Abush-Shaykh, ametuhadithia: Abu Ja´far Ahmad bin Ziyrak al-Yazdiy ametuhadithia: Nimemsikia Muhammad bin ‘Amr bin an-Nadhwr an-Naysaabuuriy[4] akisema: Nimemsikia Yahyaa bin Yahyaa akisema:

“Tulikuwa kwa Maalik bin Anas alipoingia bwana mmoja na kusema: “Ee Abu ´Abdillaah!

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[5]

Amelingana juu vipi?” Maalik akainamisha kichwa chake mpaka akaanza kutokwa na jasho. Kisha akasema: “Kulingana juu si kitu kisichofahamika. Namna haitambuliki. Ni wajibu kuamini hilo na kuuliza juu ya hilo ni Bid´ah. Mimi sikuoni vyengine isipokuwa mzushi.” Kisha kaamuru atolewe nje.”[6]

al-Bayhaqiy pia ameipokea katika “Kitaab-ul-I’tiqaad” kwa cheni hiyohiyo ya wapokezi.

adh-Dhahabiy ameitaja katika “al-‘Uluww” na akasema:

“Yahyaa bin Yahyaa, Ja’far bin ‘Abdillaah na wengineo wameipokea… Hii imethibiti kutoka kwa Maalik.”[7]

Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin ´Abdil-Haadiy amesema katika kitabu chake al-Istiwaa’:

“Swahiyh na iliyothibiti kutoka kwa Maalik.”

[1] Abu Zakariyyaa Yahyaa bin Yahyaa bin Bakr at-Tamiymiy an-Naysaabuuriy. Alikuwa mtu madhubuti kwa mujibu wa Ahmad bin Hanbal, Ibn Raahuuyah, an-Nasaa’iy na wengineo. Alifariki mnamo 226. Tazama “Tahdhiyb-ul-Kamaal” (32/31-37).

[2] Abu Bakr Ahmad bin Muhammad bin Ahmad bin ´Abdillaah bin al-Haarith al-Faqiyh at-Tamiymiy al-Aswfahaaniy. adh-Dhahabiy amesema juu yake:

“Msomaji Qur-aan mwenye kuipa nyongo dunia, mwanasarufi na Muhaddith. Alikuwa ni kiongozi kwenye kiarabu.” (Taariykh-ul-Islaam, uk. 281. Alifariki mnamo 430)

[3] Abu Muhammad ´Abdullaah bin Muhammad bin Ja´far bin Hayyaan, ambaye pia anatambulika kama Shaykh. al-Khatwiyb al-Baghdaadiy amesema juu yake:

“Abush-Shaykh mwenye kuhifadhi, imara na thabiti.”

Alifariki mwaka wa 369. Tazama “Siyar A´laam-in-Nubalaa’” (16/277-279).

[4] Abu ´Aliy Muhammad bin ´Amr bin an-Nadhwr al-Dhurashiy an-Naysaabuuriy. adh-Dhahabiy amesema juu yake:

“Alikuwa mkweli na mwenye kukubaliwa.” (Taariykh-ul-Islaam, uk. 282, alifariki 281-290)

[5] 20:05

[6] al-Asmaa’ was-Swifaat (2/305-306).

[7] Mukhtaswar-ul-´Uluww, uk. 141.

  • Muhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Allaamah ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad al-Badr
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Athar al-Mash-huur ´an-il-Imaam Maalik fiy Swifat-il-Istiwaa’, uk. 34-35
  • Imechapishwa: 29/11/2025