al-Qummiy amesema wakati alipokuwa akitafasiri Aayah ifuatayo:
وَيُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ
”Allaah anataka athibitishe haki kwa maneno Yake na akate mizizi ya makafiri.”[1]
Amesema: “Maneno ni maimamu.”[2]
Udhahiri ni kwamba anamkusudia Abu ´Abdillaah Ja´far as-Swaadiq ndiye amesema hivo.
Allaah amtakase Abu ´Abdillaah kutokana na uongo huu wa ki-Baatwiniy! Maneno ya Allaah ni yale yanayolingana Naye ambayo kwayo ameumba viumbe vyote na kuweka kwayo Shari´ah zote. Amesema (Ta´ala):
قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا
“Sema: “Endapo bahari ingelikuwa ni wino wa [kuandika] maneno ya Mola wangu, basi ingelimalizika bahari kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu ijapo tungelileta mfano wake kujaza tena.”[3]
وَلَوْ أَنَّمَا فِي الْأَرْضِ مِن شَجَرَةٍ أَقْلَامٌ وَالْبَحْرُ يَمُدُّهُ مِن بَعْدِهِ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ مَّا نَفِدَتْ كَلِمَاتُ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
”Na lau kama miti yote iliyomo ardhini ingekuwa ni kalamu na bahari [ikawa wino], na ikaongezewa juu yake bahari zengine saba, basi yasingelimalizika maneno ya Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye hekima ya yote.”[4]
[1] 8:7
[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/270).
[3] 18:109
[4] 31:27
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 218
- Imechapishwa: 13/08/2025
al-Qummiy amesema wakati alipokuwa akitafasiri Aayah ifuatayo:
وَيُرِيدُ اللَّـهُ أَن يُحِقَّ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَيَقْطَعَ دَابِرَ الْكَافِرِينَ
”Allaah anataka athibitishe haki kwa maneno Yake na akate mizizi ya makafiri.”[1]
Amesema: “Maneno ni maimamu.”[2]
Udhahiri ni kwamba anamkusudia Abu ´Abdillaah Ja´far as-Swaadiq ndiye amesema hivo.
Allaah amtakase Abu ´Abdillaah kutokana na uongo huu wa ki-Baatwiniy! Maneno ya Allaah ni yale yanayolingana Naye ambayo kwayo ameumba viumbe vyote na kuweka kwayo Shari´ah zote. Amesema (Ta´ala):
قُل لَّوْ كَانَ الْبَحْرُ مِدَادًا لِّكَلِمَاتِ رَبِّي لَنَفِدَ الْبَحْرُ قَبْلَ أَن تَنفَدَ كَلِمَاتُ رَبِّي وَلَوْ جِئْنَا بِمِثْلِهِ مَدَدًا
“Sema: “Endapo bahari ingelikuwa ni wino wa [kuandika] maneno ya Mola wangu, basi ingelimalizika bahari kabla ya kumalizika maneno ya Mola wangu ijapo tungelileta mfano wake kujaza tena.”[3]
وَلَوْ أَنَّمَا فِي الْأَرْضِ مِن شَجَرَةٍ أَقْلَامٌ وَالْبَحْرُ يَمُدُّهُ مِن بَعْدِهِ سَبْعَةُ أَبْحُرٍ مَّا نَفِدَتْ كَلِمَاتُ اللَّـهِ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَزِيزٌ حَكِيمٌ
”Na lau kama miti yote iliyomo ardhini ingekuwa ni kalamu na bahari [ikawa wino], na ikaongezewa juu yake bahari zengine saba, basi yasingelimalizika maneno ya Allaah. Hakika Allaah ni Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye hekima ya yote.”[4]
[1] 8:7
[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/270).
[3] 18:109
[4] 31:27
Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 218
Imechapishwa: 13/08/2025
https://firqatunnajia.com/158-al-qummiy-upotoshaji-wake-wa-pili-wa-al-anfaal/