Nazo ni sita:
1 – Kujisafisha kutokana na hadathi. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna swalah kwa mwenye hadathi mpaka atawadhe.”[1]
2 – Wakati. Wakati wa Dhuhr ni kuanzia jua linapopinduka mpaka kivuli cha kila kitu kiwe sawa na urefu wake.
Wakati wa ´Aswr – ambayo ndio swalah ya katikati – ni kuanzia mwisho wa wakati wa Dhuhr mpaka jua linapogeuka kuwa la njano. Kisha wakati wa chaguo unaisha. Unabaki wakati wa dharurah mpaka jua linapozama.
Wakati wa Maghrib ni mpaka pale ule msitari mwekundu utoweke.
Wakati wa ´Ishaa ni kuanzia hapo mpaka nusu ya usiku. Kisha unabaki wakati wa dharurah mpaka kuchomoza kwa alfajiri ya pili.
Wakati wa Fajr ni kuanzia hapo mpaka jua linapochomoza.
Mwenye kuleta Takbiyr ya kuingia ndani ya swalah kabla ya kutoka kwa wakati wake, basi ameiwahi swalah hiyo. Kuswali mwanzoni mwa wakati ndio bora, isipokuwa ´Ishaa na Dhuhr wakati joto ni kali.
[1] al-Bukhaariy (135) na Muslim (225).
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 22
- Imechapishwa: 04/10/2026
Nazo ni sita:
1 – Kujisafisha kutokana na hadathi. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna swalah kwa mwenye hadathi mpaka atawadhe.”[1]
2 – Wakati. Wakati wa Dhuhr ni kuanzia jua linapopinduka mpaka kivuli cha kila kitu kiwe sawa na urefu wake.
Wakati wa ´Aswr – ambayo ndio swalah ya katikati – ni kuanzia mwisho wa wakati wa Dhuhr mpaka jua linapogeuka kuwa la njano. Kisha wakati wa chaguo unaisha. Unabaki wakati wa dharurah mpaka jua linapozama.
Wakati wa Maghrib ni mpaka pale ule msitari mwekundu utoweke.
Wakati wa ´Ishaa ni kuanzia hapo mpaka nusu ya usiku. Kisha unabaki wakati wa dharurah mpaka kuchomoza kwa alfajiri ya pili.
Wakati wa Fajr ni kuanzia hapo mpaka jua linapochomoza.
Mwenye kuleta Takbiyr ya kuingia ndani ya swalah kabla ya kutoka kwa wakati wake, basi ameiwahi swalah hiyo. Kuswali mwanzoni mwa wakati ndio bora, isipokuwa ´Ishaa na Dhuhr wakati joto ni kali.
[1] al-Bukhaariy (135) na Muslim (225).
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 22
Imechapishwa: 04/10/2026
https://firqatunnajia.com/14-sharti-za-swalah-twahara-na-wakati/