Katika sifa za mke mwema ni kwamba hatoi siri za mume wake na yale mambo yanayowahusu wao tu. Hata kama kutatokea kutengana/kuachana na kutokuafikiana, basi ni lazima kwao wote wawili wamche Allaah (Jalla wa ´Alaa) juu ya suala hili. Kuhusiana na hili amepokea Imaam Ahmad katika “al-Musnad”[1] yake kupitia Amsaa´ bint Yaziyd ambaye ameeleza kwamba alikuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanaume na wanawake walikuwa wamekaa kwake. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Pengine mwanaume akasema aliyofanya na mke wake. Pengine mwanamke akasema aliyofanya na mume wake.” Wakanyamaza kimya. Nikasema: “Ni kweli, ee Mtume wa Allaah. Wanawake wanafanya hivyo. Wanaume wanafanya hivyo.” Akasema: “Msifanye hivyo. Hili linafanana na Shetani ambaye amekutana na mwanamke wa kishetani barabarani akaanza
kujamiiana naye na huku watu wanatazama.”
Amesema:
”Wanawake wanafanya hivyo. Wanaume wanafanya hivyo.”
Ameanza na wanawake kwanza kwa sababu hili hufanywa sana kati yao na huwa kwa mara chache sana kati ya wanaume. Mwanamke huongea na marafiki zake na maswahiba zake kuhusu mambo kama hayo ya binafsi. Wengi katika wao hawajali kuongea siri za mume na mambo yao binafsi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
“Hili linafanana na Shetani ambaye amekutana na mwanamke wa kishetani barabarani akaanza kujamiiana naye na huku watu wanatazama.”
Bi maana mwanamke na mwanaume wenye sifa kama hii na wanafichukua siri zao ni kama Shetani wa kiume ambaye amekutana na Shetani wa kike barabarani na akajamiiana naye na huku watu wanatazama.
[1] 27583. Ni Swahiyh kupitia Hadiyth zingine kwa mujibu wa Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (2022). Tazana ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (2011).
- Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 42-44
- Imechapishwa: 20/08/2018

Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Swifaat-uz-Zawjah as-Swaalihah, uk. 42-44
Imechapishwa: 20/08/2018
https://firqatunnajia.com/13-mke-mwema-hatoi-siri-za-mume-wake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)