12. Mfungaji kutumia sprei za kuondosha harufu mbaya mdomoni

Swali: Katika maduka ya dawa kuna manukato maalum kwa ajili ya mdomo. Manukato hayo ni ya sprei. Je, inafaa kuitumia mchana wa Ramadhaan kwa ajili ya kuondosha harufu mbaya mdomoni?

Jibu: Hatujui ubaya kwa mfungaji na mtu mwengine kutumia kitu cha kuondosha harufu mbaya kutoka mdomoni muda wa kuwa kitu hicho ni kisafi na halali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ashyaa´ laa tufsid-is-Swawm, uk. 12
  • Imechapishwa: 01/04/2021