Makadirio ya Allaah ni yale Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) aliyowakadiria viumbe Wake. Kila kitu chenye kupitika katika ulimwengu huu kimekadiriwa. Hakuna chochote kinachopitika isipokuwa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) amekikadiria. Allaah alikijua, akakikadiria, akakiandika na akatenga wakati wake wa kutokea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kitu cha kwanza alichoumba Allaah ni kalamu. Akaiambia: “Andika!” Kukadiriwa yote yatayokuwepo hadi siku ya Qiyaamah.”[1]
Ikaandika kwenye Ubao uliohifadhiwa. Hakuna chochote kinachopitika isipokuwa kimekadiriwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kimeshapangiwa muda wake wa kutokea ambao hautoharakishwa wala kucheleweshwa. Kila kitu kimeandikwa kwenye Ubao uliohifadhiwa.
Kuamini makadirio ni moja katika zile nguzo sita za imani. Jibriyl (´alayhis-Salaam) amesema:
“Imani ni nini?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akajibu: “Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, siku ya Mwisho na kuamini Qadar, kheri na shari yake.”[2]
Akasema kuwa kuamini Qadar ni moja katika zile nguzo sita za imani. Allaah (Ta´ala) amesema:
“ina kul…qadar” 54:49
Imepokelewa katika Hadiyth Swahiyh ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amekadiria makadirio miaka elfukhamsini kabla ya kuumba mbingu na ardhi na ´Arshi Yake ilikuwa juu ya maji.”[3]
Hakuna chochote kikubwa na kidogo kinachopitika katika ulimwengu huu isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amekikadiria.
[1] Abu Daawuud (2700), at-Tirmidhiy (2155) na Ahmad (22705) kupitia kwa ´Ubaadah bin as-Swaamitw. Hadiyth ni Swahiyh.
[2] Muslim (93) na Ahmad (367).
[3] Muslim (2653).
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 431-432
- Imechapishwa: 14/08/2019
Makadirio ya Allaah ni yale Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) aliyowakadiria viumbe Wake. Kila kitu chenye kupitika katika ulimwengu huu kimekadiriwa. Hakuna chochote kinachopitika isipokuwa Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) amekikadiria. Allaah alikijua, akakikadiria, akakiandika na akatenga wakati wake wa kutokea. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Kitu cha kwanza alichoumba Allaah ni kalamu. Akaiambia: “Andika!” Kukadiriwa yote yatayokuwepo hadi siku ya Qiyaamah.”[1]
Ikaandika kwenye Ubao uliohifadhiwa. Hakuna chochote kinachopitika isipokuwa kimekadiriwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kimeshapangiwa muda wake wa kutokea ambao hautoharakishwa wala kucheleweshwa. Kila kitu kimeandikwa kwenye Ubao uliohifadhiwa.
Kuamini makadirio ni moja katika zile nguzo sita za imani. Jibriyl (´alayhis-Salaam) amesema:
“Imani ni nini?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akajibu: “Ni kumwamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, siku ya Mwisho na kuamini Qadar, kheri na shari yake.”[2]
Akasema kuwa kuamini Qadar ni moja katika zile nguzo sita za imani. Allaah (Ta´ala) amesema:
“ina kul…qadar” 54:49
Imepokelewa katika Hadiyth Swahiyh ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah amekadiria makadirio miaka elfukhamsini kabla ya kuumba mbingu na ardhi na ´Arshi Yake ilikuwa juu ya maji.”[3]
Hakuna chochote kikubwa na kidogo kinachopitika katika ulimwengu huu isipokuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amekikadiria.
[1] Abu Daawuud (2700), at-Tirmidhiy (2155) na Ahmad (22705) kupitia kwa ´Ubaadah bin as-Swaamitw. Hadiyth ni Swahiyh.
[2] Muslim (93) na Ahmad (367).
[3] Muslim (2653).
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 431-432
Imechapishwa: 14/08/2019
https://firqatunnajia.com/04-qadar-imeandikwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)