Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna matendo yoyote yaliyo safi zaidi kwa Allaah (‘Azza wa Jall), wala yenye ujira mkubwa zaidi kuliko kheri anayofanya mtu katika siku kumi za al-Adhwhaa.” Wakauliza: ”Wala jihaad katika njia ya Allaah?” Akasema: “Wala jihaad katika njia ya Allaah; isipokuwa mtu ambaye ametoka na nafsi yake na mali yake, kisha hakurudi na chochote kutoka humo.”[1]
Ameipokea ad-Daarimiy kwa cheni ya wapokezi nzuri.
Hakika kuzipata siku hizi kumi ni neema kubwa kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa mja wake, kwa sababu amepata msimu miongoni mwa misimu ya utiifu ambayo inamsaidia – kwa tawfiyq ya Allaah – katika kupata thawabu na kunufaika na ujira. Hivyo basi ni lazima kwa muislamu ahisi neema hii, akumbuke ukubwa wa thawabu ya matendo ndani yake na kuzitumia vizuri nyakati hizi. Aidha ni vyema kuonyesha ubora wa siku hizi kuliko siku nyingine kwa kuzidisha utiifu. Hii ilikuwa ni tabia ya Salaf wa ummah huu, kama alivosema Abu ´Uthmaan an-Nahdiy (Rahimahu Allaah):
“Walikuwa wakitukuza makumi matatu: kumi la mwisho la Ramadhaan, kumi la mwanzo la Dhul-Hijjah na kumi la mwanzo la Muharram.”[2]
[1] al-Bukhaariy (02/457), Abu Daawuud (07/103), at-Tirmidhiy (03/463), Ibn Maajah (01/550) na Ahmad (3/298). Tamko ni la at-Tirmidhiy.
[2] Latwaa’if-ul-Ma’aarif, uk. (39) na Haafidhwh ameandika wasifu wa Abu ´Uthmaan an-Nahdiy katika ”Tahdhiyb wat-Tahdhiyb (06/249). Alikufa mwishoni mwa karne ya kwanza.
- Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 6
- Imechapishwa: 04/05/2025
Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesimulia ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna matendo yoyote yaliyo safi zaidi kwa Allaah (‘Azza wa Jall), wala yenye ujira mkubwa zaidi kuliko kheri anayofanya mtu katika siku kumi za al-Adhwhaa.” Wakauliza: ”Wala jihaad katika njia ya Allaah?” Akasema: “Wala jihaad katika njia ya Allaah; isipokuwa mtu ambaye ametoka na nafsi yake na mali yake, kisha hakurudi na chochote kutoka humo.”[1]
Ameipokea ad-Daarimiy kwa cheni ya wapokezi nzuri.
Hakika kuzipata siku hizi kumi ni neema kubwa kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) kwa mja wake, kwa sababu amepata msimu miongoni mwa misimu ya utiifu ambayo inamsaidia – kwa tawfiyq ya Allaah – katika kupata thawabu na kunufaika na ujira. Hivyo basi ni lazima kwa muislamu ahisi neema hii, akumbuke ukubwa wa thawabu ya matendo ndani yake na kuzitumia vizuri nyakati hizi. Aidha ni vyema kuonyesha ubora wa siku hizi kuliko siku nyingine kwa kuzidisha utiifu. Hii ilikuwa ni tabia ya Salaf wa ummah huu, kama alivosema Abu ´Uthmaan an-Nahdiy (Rahimahu Allaah):
“Walikuwa wakitukuza makumi matatu: kumi la mwisho la Ramadhaan, kumi la mwanzo la Dhul-Hijjah na kumi la mwanzo la Muharram.”[2]
[1] al-Bukhaariy (02/457), Abu Daawuud (07/103), at-Tirmidhiy (03/463), Ibn Maajah (01/550) na Ahmad (3/298). Tamko ni la at-Tirmidhiy.
[2] Latwaa’if-ul-Ma’aarif, uk. (39) na Haafidhwh ameandika wasifu wa Abu ´Uthmaan an-Nahdiy katika ”Tahdhiyb wat-Tahdhiyb (06/249). Alikufa mwishoni mwa karne ya kwanza.
Muhusika: Shaykh ´Abdullaah bin Swaalih al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahaadiyth ´Ashrah Dhil-Hijjah wa Ayaam-it-Tashriyq, uk. 6
Imechapishwa: 04/05/2025
https://firqatunnajia.com/02-hadiyth-hakuna-matendo-yoyote-yaliyo-safi-zaidi-kwa-allaah/